NAIBU WAZIRI PINDA ATAKA USHIRIKIANO MKUBWA KULETA MAGEUZI SEKTA YA ARDHI

NA ANTHONY ISHENGOMA-WANMM

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Geofrey Pinda ameahidi kushirikiana na watendaji wakuu wa Wizara pamoja na maofisa wa sekta ya ardhi nchini ili kuhakikisha sekta hiyo hapa Nchini inasimamiwa vizuri na kutoa matokeo makubwa kwa wananchi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akimkabidhi Naibu wake Bw.Geofrey Pinda kadi ya pongezi iliyosainiwa na viongozi wakuu wa Wizara mapema leo katika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dodoma, kulia kwake ni Mhandisi Anthony Sanga Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi akifuatiwa na Bi.Lucy Kabyemela Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Naibu Waziri Pinda amesema hayo leo tarehe 6, Machi 2023 alipowasili kwa mara ya kwanza tangu alipotelewa kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo hivi karibuni na kukutana na Menejimenti ya Wizara kwa ajili kufahamiana, lakini pia kupata fursa ya kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Wizara ya Ardhi.

Kabla ya kukutana na Menejimenti ya Wizara awali Naibu Waziri Pinda alipokelewa kwa shangwe na watumishi wa Wizara yake mpya waliojitokeza kwa wingi kwa ajili ya mapokezi yake na wote walisikika wakiimba wimbo wa kuwa na imani kubwa na yeye ambapo pia aliwasilimia katika ari kubwa watumishi hao.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga muda mfupi baada ya kupolewa Wizarani hapo tayari kwa majukumu mapya ya kikazi.

Kiongozi huyo mpya katika Wizara ya Ardhi alisema kuwa ni matarajio yake kuwa atapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa watendaji wa Wizara ili aweze kumsaidia Waziri wake lakini pia kukidhi matarajio ya wananchi hususani baada ya serikali kufanya mabadiliko ya uongozi katika sekta mbalimbali serikalini.

Akiongelea suala la wananchi kuchangia mapato ya Serikali kupitia pango la ardhi Naibu Waziri Pinda alibainisha kuwa kwa sasa inawezekana kuna changamoto katika mfumo uliopo hivyo Wizara itahakikisha inafanya maboresho kujenga mfumo rafiki utakaowezesha wananchi kulipa kodi ya pango la ardhi bila usumbufu wowote.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Bi. Lucy Kabyemela muda mfupi baada ya kupolewa Wizarani hapo tayari kwa majukumu mapya ya kikazi.

Aidha, Pinda aliongeza kuwa katika kukabiliana na changamoto iliyopo ya kimfumo juhudi zilizopo ni kushirikisha wananchi ili waweze kutambua umuhimu wa kulipa kodi ya ardhi lakini pia kuonesha umuhimu wa mchango wetu katika katika kukuza pato la taifa kwani ardhi ndiyo kila kitu.
Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akimkaribisha Naibu wake Bw. Geofrey Pinda kwa mara ya kwanza ofisini kwake muda mfupi baada ya kupolewa Wizarani hapo tayari kwa majukumu mapya ya kikazi.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa atatumia fursa yake kujenga upendo miongoni mwa watumisha pamoja na kuwapa motisha na kutambua utaalamu wao ili watumishi wa sekta ya ardhi katika ngazi zote waweze kujenga umoja katika utekelezaji kazi kama hatua muhimu ya kuleta mageuzi kiutendaji katika sekta ya ardhi kote nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news