Rais Dkt.Mwinyi aishukuru ZMBF kwa kuunga mkono jitihada za Serikali

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa shukrani kwa niaba ya Serikali kwa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) kwa kuunga mkono jitihada za Serikali kwa maeneo waliyolenga hususani uwezeshaji wa wanawake na vijana kiuchumi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizindua Mpango Mkakati wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZBMF), uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Fondation (ZMBF) ambaye ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Maria Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana na kulia kwa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,Mhe. Masoud Ali Mohammed.(Picha na Ikulu).

Ni wanaojishughulisha na kilimo cha mwani kwa kuwapa mafunzo na vifaa walivyotafuta kwa juhudi zao, ulinzi wa watoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na kukabaliana na tatizo la udumavu linatokana na lishe duni. 

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Machi 20, 2023 alipozindua Mpango Mkakati wa Miaka Mitatu wa ZMBF na mradi wa taulo za kike wa Tumaini katika Maadhimisho ya Mwaka mmoja wa ZMBF yaliyofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport jijini Zanzibar. 
Katika hatua nyingine, Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali itaendelea kutekeleza programu mbalimbali za zao la mwani Unguja na Pemba. 

Ameishukuru ZMBF kwa juhudi za mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto hapa Zanzibar kwa kulifanya kuwa ajenda na sauti ya waathirika kupata uzito.Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa, Serikali inaunga mkono juhudi hizo katika jambo hilo kuliondoa nchini. 

Naye Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi amesema, ZMBF imejikita kuwainua akina mama na vijana kiuchumi.Sambamba na kuwahakikishia watoto wa kike na wa kiume ulinzi dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa kulinda utu wao pamoja na kuwawezesha watoto wa kike kufurahia utoto wao wakiwa katika siku za ada za mwezi kwa kuwapatia taulo za kike kupitia mradi wa Tumaini. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news