Wachimbaji nane wafariki Geita

NA DIRAMAKINI

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa ajali iliyoua wachimbaji wadogo nane ambao wamefukiwa na kifusi.

Ni katika Kijiji cha Igando kilichopo Kata ya Magenge wilayani Geita ambapo wachimbaji hao walikuwa wakiendelea na shughuli za uchimbaji kwenye eneo lisilo rasmi.

Amesema, wachimbaji hao walikutwa na umauti huo majira ya saa tisa usiku wa kuamkia Machi 11, 2023, baada ya mvua kubwa kunyesha eneo jirani na maporomoko ya maji kuvamia mashimo walipokuwa wakichimba.

Kamanda Jongo aliwataja waliofariki ni Juma Pamba (42), Akili Anthony (40), Samwel John (25), Juma Swalele (50), Simon Mabula (40) Kamala Nyambogo (30), Bahati Nyambogo (25), pamoja na Juma Sumuni (53) na wanatokea Ipalamasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news