Waziri Dkt.Mabula awataka wanawake kujiamini

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula amewataka wanawake nchini kujiamini wakati wa kutekeleza majukumu yao. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima wakipokea maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Kwadeko wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza tarehe 8 Machi, 2023.(Picha na WANMM).

Dkt.Mabula amesema hayo Machi 8,2023 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Kwadeko wilayani Kwimba mkoani Mwanza. 

Amesema, wanawake wanatakiwa kufanya kazi zao huku wakielewa kuwa juu yao yupo mwanamke shujaa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan aliyemueleza kuwa ameonesha kuwa wanawake wanaweza. 
Askari wa kikosi cha Zimamoto akionesha namna ya kuzima moto kwa kutumia ‘Fire Blangeti’ wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya Kwadeko wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza tarehe 8 Machi 2023.

"Tulioko katika nafasi tunatakiwa kuangalia watangulizi wetu walichofanya kama vile akina Mongela na Asha-Rose Migiro na kila mwanamke anayepewa nafasi ya uongozi mahali fulani, anatakiwa kujiamini kwa kuwa wanawake wamemuweka pale," amesema Dkt.Mabula. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (Wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima (kulia) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Kushoto) wakipokea maandamano wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Kwadeko wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza tarehe 8 Machi 2023.

Akigeukia upande wa Sekta ya Ardhi, Dkt. Mabula alielezea azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama mwanamke kuonesha kuwajali wananchi hasa pale alipoamua kutoa msamaha wa riba kwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi ambapo msamaha huo ulianza Julai hadi Desema, mwaka 2022 na baada ya muda huo kuisha aliongeza hadi Aprili 30, mwaka huu. 
Watumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika viwanja vya Kwadeko wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza tarehe 8 Machi 2023. 

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, uamuzi huo wa Rais Dkt.Samia unalenga kuwapa nafuu watanzania bila kujali jinsia zao ambapo alitoa wito kwa wadaiwa wote kutumia fursa iliyotolewa kulipa madeni na kusema muda huo ukipita hakuna haja ya kumlaumu rais wala wizara ya ardhi. 
Sehemu ya wanawake wakifurahia wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Kwadeko wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza tarehe 8 Machi 2023.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima aliyekuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ya Siku ya Wanawake Duniani kimkoa alikemea masuala ya ukatili kwa watoto pamoja na jinsia na kusisitiza kuwa, akina mama wana wajibu wa kuhakikisha wanakuwa na utaratibu wa kufuatilia hali za watoto wao kwa lengo la kutengeneza kizazi chenye usalama. 

"Kuwepo utaratibu wa kutoa elimu kwa jamii katika masuala ya yanoathiri akina mama katika jamii na kuanzia ngazi za chini ili kuitengenezea jamii uelewa,’’amesema Malima. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Ardhi walioshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika viwanja vya Kwadeko wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza tarehe 8 Machi 2023. 

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Mkoa wa Mwanza yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali na yaliambatana na michezo sambamba na kutoa misaada kwa akina mama wakiwemo wajawazito.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news