Waziri Mkuu atembelea mabanda mbalimbali Maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu wametembelea mabanda ya taasisi pamoja na wadau yakiongozwa na banda la Wizara ya Afya kwa lengo la kujua huduma zinazotolewa katika taasisi hizo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani tarehe 24 Machi, 2023.
Miongoni mwa mabanda yaliyokuwepo ni pamoja na banda la SUA Apopo ambalo linatoa huduma ya upimaji wa Kifua Kikuu kwa kutumia panyabuku, Clinic tembezi inayopima Kifua Kikuu (Gari) ambapo kuna chumba cha daktari, chumba cha X-Ray na chumba cha maabara. 
Maadhimisho hayo ya Kifua Kikuu hufanyika kila Mwaka tarehe 24 ambapo mwaka huu yamefanyika Kitaifa katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu yenye kauli mbiu isemayo “Kwa Pamoja Tumaweza Kutokomeza Kifua Kikuu Nchini Tanzania”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news