Benki kuuza mali ya mdhamini

NA BASHIR YAKUB

APRILI Mosi,2023 Mahakama ya Rufaa imesisitiza kuwa, unapomdhamini mtu kwa kuweka mali yako rehani ili uliyemdhamini achukue mkopo basi unatakiwa kujua kuwa hatia yako na huyo uliyemdhamini ni sawa pale anaposhindwa kulipa mkopo.

Mahakama imesema hivyo wakati ikitafsiri kifungu cha 78 cha Sheria ya Mikataba katika Rufaa Na.376/2019 kati ya Partrick Edward Mushi vs Commercial Bank of Africa.
Kwa hiyo wanaodhamini wanatakiwa kujua kuwa kudhamini ni sawa na kukopa. Wewe uliyedhamini na huyo uliyemdhamini akachukua hela nyote ni sawa likitokea la kutokea.Usije kutegemea kuwa utasema mimi ni mdhamini tu, laa hasha, nyote ni sawa.

Na mahakama inasisitiza kuwa endapo uliyemdhamini atashindwa kulipa mkopo basi yafaa mali yako iuzwe mara moja, huu ndio msimamo.

Kwa msimamo huu ni muhimu sana kabla hujamdhamini mtu kujiridhisha na kila kitu ikiwemo uwezo wake wa kulipa, biashara zake, uaminifu wake,utu na mahusiano yenu nk.

Katika mambo ambayo hutakiwi kukurupuka ni hili. Tunajua wadhamini nao hupewa fungu mkopo ukitoka, lakini yawezekana hilo fungu ndiyo pesa ya mauzo ya mali yako.Nirudie tena kuwa hakuna tofauti kati ya mdhamini na mkopaji deni linaposhindwa kulipwa.

Mwandihi wa Makala haya, Bashir Yakub ni Wakili anapatikana kupitia simu +255714047241.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news