Mtume Bethania Simon Mpembwa awapa tabasamu watu kupitia upendo wa Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie

NA DIRAMAKINI

UPENDO wa Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie wa Kanisa la GeorDavie Ministries International (Ngurumo ya Upako) lililopo Kisongo jijini Arusha ambao umetawaliwa na moyo wa utoaji kwa makundi mbalimbali nchini, umeendelea kusambaa hadi kwa watoto wake wa kiroho ambapo,Askofu Mkuu wa Kanisa la Neema ya Kitume, Mtume Bethania Simon Mpembwa amejikuta akigawa sadaka zote kwa ajili ya waumini wake kwenda kufurahia Sikukuu ya Pasaka. 
Dkt.GeorDavie ndiye mtumishi wa Mungu anayetambulika kwa utoaji misaada na zawadi mbalimbali kwa watu wote (Wanangurumo na wasiokuwa waumini wa Ngurumo Ya Upako) nchini.
Kupitia ibada iliyofanyika Aprili 9, 2023 katika Kanisa la Neema ya Kitume lililopo Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtume Bethania Simon Mpembwa alibainisha kuwa, ni heri yeye na familia yake kula wali maharage na nyanya chungu huku wenye mahitaji mbalimbali wakifurahia kupitia kile kidogo alichogusa maisha yao, na huo ndiyo moyo wa upendo alionao Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie kwa watu wote.

Amesema, kupitia ibada hiyo kubwa, "Kila mtu ameruzukiwa kwa kiwango chake ili kufurahia pamoja Pasaka hii 2023, ni kwa fundisho la Baba Nabii Mkuu Dkt.Geordavie na matamko aliyonipatia.

"Pamoja tuna madeni, pamoja tuna shida,pamoja tuna changamoto pamoja tuna uhitaji, lakini kwa fundisho la Nabii Mkuu, Nabii Geordavie, Balozi na Baba yetu anafundisha na anasema, wewe kula wakati wenzako hawali, ni kana kwamba na wewe umeshinda njaa, Pasaka hii ya leo nmefanya jambo hili ili kila mmoja aweze kufurahia sikukuu.

"Kama mafundisho ya onesha upendo kwa watu, jali watu haina maana wewe kula wakati wengine wana njaa. Tumegawa ruzuku, sadaka zote zilizopatikana katika ibada ya leo, zote nimezigawa ruzuku kwa waumini, sema what God can do no man can do, Mungu akubariki sana, tuoneshe upendo kwa watu hata kwa waumini wetu tunaowaongoza, wahitaji hapa kanisani tuoneshe upendo na Mungu atatutokelezea, kutoa si kitu kidogo, ni roho na ni moyo na sisi tumeupokea moyo huo,"amefafanua Mtume Bethania.
Pia amesema Aprili 25, mwaka huu wakati wa siku ya kuzaliwa kwa Nabii Mkuu Dkt.Geordavie litafanyika tukio lingine muhimu kwa ajili ya kusherehekea siku hiyo muhimu.
Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie wa Kanisa la GeorDavie Ministries International (Ngurumo ya Upako) mbali na kutoa mitaji ya fedha, mahitaji ya msingi kwa jamii na magari kwa nyakati tofauti,pia amekuwa akiguswa na hali waliyonayo baadhi ya waumini wake na wasio waumini wake hivyo kuamua kuwasaidia kwa kila njia.

Pia,Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie mbali na kusaidia waumini, jamii lakini pia amekuwa akiunga mkono juhudi mbalimbai za maendeleo za Serikali ikiwemo kutoa michango katika sekta za afya, elimu, uchumi na nyinginezo.

Aidha, mara nyingi Nabii Mkuu amekuwa akieleza sababu za kutoa misaada hiyo katika sekta mbalimbali ikiwemo kusaidia vituo vya kulelea watoto yatima na wenye mahitaji mbalimbali nchini kuwa ni jambo la baraka.

“Mimi ninaona ni jambo zuri na la baraka kwa kufanya hivi hasa tunapokuwa tumefanikiwa katika maisha ni vizuri tuwakumbuke watu wadogo tukijua ndiko tulikotoka,na watu wenye uwezo wawakumbuke watu wadogo. Watu wadogo kwa kweli ni watu wanafanya kazi mchana na usiku ndio wanajitahidi,ndio wanabeba Taifa hili kwa asilimia kubwa sana,kwa hiyo tuwakumbuke vijana wetu wadogo wainuke,”Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie aliyabainisha hayo hivi karibuni jijini Arusha wakati akitoa fedha kwa wafanyabiashara wa Soko la Kisongo wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news