Rais Dkt.Samia ampa tano mwanariadha Gabriel Geay

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amempongeza mwanariadha wa Tanzania, Gabriel Gaey ambaye ameshika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon 2023 zilizofanyika Boston Massachusetts nchini Marekani.

Mtanzania Gaey katika mbio hizo ametumia saa 2:06:04 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Mkenya Evans Chebet aliyetumia saa 2:05:54.

Rais Dkt. Samia ametoa pongezi hizo leo Aprili 17, 2023 kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii ambapo amesema, mafanikio hayo yameipa heshima Tanzania.

"Nakupongeza Gabriel Gerald Geay kwa kuwa mshindi wa pili katika Mashindano ya Riadha ya Kimataifa ya Boston yaliyofanyika leo nchini Marekani. Jitihada zako zimeijengea heshima Tanzania. Nakutakia kheri katika kusonga mbele zaidi. Serikali itaendelea kuwaunga mkono wanamichezo,"amefafanua Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news