RUWASA yaendeleza shangwe ya maji Musoma Vijijini

NA FRESHA KINASA

IMEELZEWA kuwa,maji ya Ziwa Victoria yanaendelea kusambazwa katika Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara. Ambapo utekelezaji wa Mradi wa maji ya bomba wa Chumwi- Mabuimerafuru unaendelea vizuri chini ya usimamizi mzuri wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ili kuwasogezea huduma hiyo wananchi.
Jimbo la Musoma Vijijini lenye kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68 limezungukwa na Ziwa Victoria. Ambapo wananchi wa jimbo hilo wameendelea kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wao Prof. Sospeter Muhongo kwa juhudi zao za dhati za kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao. 

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini leo Aprili Mosi, 2023 imeeleza kuwa, "Ujenzi unaoendelea kwa wakati huu ni:ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 300,000 Kijijini Mabuimerafuru. ujenzi wa vioski vya maji kwenye Vijiji vya Chumwi na Mabuimerafuru. 

"Mradi huu una thamani ya shilingi bilioni 1.7 na umepangwa kukamilishwa kabla ya Julai 30,2023. Baadae, sehemu ya pili ya Mradi huu (LOT II) ni ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji kwenye vijiji vya Lyasembe na Murangi," imesema taarifa hiyo.

TAARIFA YA MIRADI MINGINE :


Pia taarifa hiyo imeeleza miradi mingine ya maji."Mradi wa Tsh bilioni 4.75 wa kusambaza maji ya bomba kwenye Kata za Tegeruka (Vijiji 3) na Mugango (Vijiji 3) unakaribia kuanza."

"Mkandarasi ameishapatikana, na taratibu za mkataba zinakamilishwa.Maji ya Kata hizi 2 yatatoka kwenye Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama ambalo limepangwa kukamilika kabla ya tarehe 30 Juni 2023."
"Usanifu wa miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye Kata za Busambara na Kiriba unakaribia kukamilika.Kata hizi 2 zitasambaziwa maji kutoka kwenye Tenki la mlima KONG lenye ujazo wa LITA 500,000. Maji ya tenki hili yatatolewa kwenye bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama.

"Fedha za usambazaji wa maji ya bomba kwenye Kata za Busambara na Kiriba zipo, na utekelezaji utaanza hivi karibuni, Julai 2023.

"Musoma Vijijini tunaendelea kuishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutusambazia maji ya bomba vijijini mwetu, asante sana,"imeeleza.
DIRAMAKINI imezungumza kwa simu na Sauda Bwire ambaye ni Mkazi wa Musoma Vijijini ambapo amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Dkt. Samia Hassan imeonesha dhamira ya dhati ya kuwasaidia Wanawake hasa kuwapa urahisi wa kupata huduma ya maji safi na salama kwa ukaribu zaidi hatua ambayo amesema inamanufaa makubwa kwa maendeleo yao.

"Nampongeza Rais Dkt. Samia Hassan na Mheshimiwa Mbunge Prof. Muhongo hii miradi ya maji tunayoiona jimboni mwetu ni kutokana na juhudi zao na dhamira njema ya kumtua mama ndoo kichwani."amesema Sauda na kuongeza.

"Kiukweli maji yakiwa karibu inatupa wepesi kina mama kufanya kazi nyingine za maendeleo badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji. Mungu ambariki Mbunge Prof. Muhongo kwa kazi nzuri ya kusimamia maendeleo yetu lakini pia Rais kwa kutoa fedha za miradi ya maji ili kumtua mama ndoo kichwani Mungu ampe maisha marefu na afya njema,"amesema Sauda Bwire. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news