Tumejipanga vema kustawisha Sekta ya Utamaduni,Sanaa na Michezo-Waziri Dkt.Chana

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa wizara yake itaendelea kusimamia na kuendeleza Sekta ya Utamaduni,Sanaa na Michezo kutokana na umuhimu na mchango wake katika maendeleo ya nchi na kwa mwananchi mmoja mmoja.

Amesema sekta hizo zina nguvu kubwa ya ushawishi, uhamasishaji na ustawishaji wa jamii na maendeleo ya nchi kupitia ajira, utalii, kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, mtangamano baina ya nchi na nchi kupitia diplomasia.
Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa Majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wadau wa Sekta Binafsi uliofanyika Machi, 30, 2023 jijini Dar es Salaam.

“Kipekee kabisa namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Sekta za Wizara. Katika uongozi wake kumekuwa na uwekezaji mkubwa katika Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo” Amesema.

Amesema Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo zinajulikana kama nguvu laini hapa nchini na zimekuwa na mvuto mkubwa kwa makundi mbalimbali ya jamii hususan vijana ambao ndio wanaunda sehemu kubwa ya nguvu kazi ya nchi.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameeelza kuwa taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa ya mwaka 2021 inaonesha kuwa Sekta ya Sanaa na burudani iliongoza kwa ukuaji wa wastani wa asilimia 19.4 na mchango wake katika uchumi wa asilimia 0.3.

Amesisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuandaa Mkakati wa Maendeleo ya Michezo na kuendelea kufanya mapitio ya Sera, Sheria zinazosimamia Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo pia inaendelea na ukarabati na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya michezo.

Aidha, amesema Sekta Binafsi imekua na mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya michezo, ufadhili wa Timu za mpira wa miguu kwa upande wa wanawake na wanaume, ufadhiliwa Ligi Kuu ya Tanzania, ujenzi wa miundombinu na uendelezaji wa vipaji vya Sanaa na Utamaduni.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Othman Yakubu akizungumza wakati wa mkutano huo amesema kuwa Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imekua na mchango mkubwa katika kukuza ajira na Pato la Taifa hapa nchini kwa kuwa ni Sekta inayoshughulika na Watanzania wote.

Ameeleza kuwa baadhi ya nchi Sekta hizo ndizo zinazopewa kipaumbele kutokana na mchango wake katika uchumi akibainisha kuwa baadhi ya nchi ikiwemo Afrika ya Kusini zimetoa kipaumbele kikubwa kwenye eneola Ubunifu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news