Tanzania, Slovenia zadhamiria kuimarisha, kukuza diplomasia

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia, Mhe. Tanja Fajon na ujumbe wake amewasili nchini Aprili 13,2023 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia, Mhe. Tanja Fajon yakiendelea.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha na kukuza uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kisiasa kati ya Tanzania na Slovenia sambamba na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Waziri Fajon katika siku yake ya kwanza nchini amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax jijini Dodoma, ambapo mazunguzo yao yalijikita kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kuanisha maeneo mapya ya ushirikiano kati ya Tanzania na Slovenia. 

Mazungumzo hayo pia yalihusisha uandaaji wa mazingira na utaratibu wa kusainiwa kwa Hati za Makubaliano katika maeno mapya ya ushirikiano yaliyoainishwa. 

Maeneo mapya ya ushirikiano yaliyoibuliwa wakati wa mazungumzo hayo ni uzalishaji dawa (pharmaceuticals), usimamizi wa rasilimali maji, utunzaji wa mazingira, ulinzi na usalama, uchumi wa buluu, sayansi na teknolojia, kilimo, Elimu,biashara na uwekezaji. 

Mbali na hayo Waziri Dkt. Tax alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Fajon kuhusu juhudi zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mafanikio yaliyopatikana nchini kutokana na juhudi hizo ikiwemo kupatikana kwa maridhiano ya kisiasa, kuimarika kwa Demokrasia, Haki za Banadamu, uhuru wa vyombo vya habari na uzingatiwaji wa usawa wa jinsia katika maendeleo.
Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Slovenia Mhe. Tanja Fajon wakiwa katika picha ya pamoja punde baada kuwasili Wizarani Mtumba jijini Dodoma.

Waziri Fajon kwa upande wake ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa hatua kubwa iliyofikiwa katika kuboresha mazingira ya Demokrasia na Utawala Bora nchini sambamba na kuendelea kusimamia vyema maendeleo ya uchumi licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali duniani zinazo dhoofisha ustawi wa uchumi. 

Ziara hii ni muendelezo wa matokeo ya juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita za kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Mataifa mengine duniani. 

Waziri Fajon akiwa nchini anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Viongozi mbalimbali Serikalini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news