Waziri Dkt.Chana atoa maagizo

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amezielekeza taasisi zilizo chini ya wizara yake zitoe mafunzo kwa wadau wake ili waweze kuelewa masuala mbalimbali zikiwemo fursa zilizopo katika Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mhe. Balozi Pindi Chana ametoa maelekezo hayo jijini Dar es Salaam wakati akifanya majumuisho ya Kikao cha Majadiliano Kati ya Wizara na Wadau wa Sekta Binafsi kilichorikisha Baraza la Biashara la Taifa (TNBC).

" Vikao na wadau ni muhimu sana katika kujenga uelewa wa pamoja na kusaidiana katika kutatua changamoto, hivyo Serikali chini ya Rais Dkt. Samia imedhamiria kuendeleza Sekta hizi ambazo ni muhimu sana kwa Wananchi," amesema Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Saidi Yakubu amesema, wizara inaendelea kuboresha muundo wa utekelezaji wa Matamasha mbakinbali ili yaongeze tija na kushirikisha Wasanii wengi.

Ameongeza kuwa, mwaka 2024,Tanzania na China zitakua zinatimiza miaka 60 ya ushirikiano, hivyo zimekubaliana kufanya shughuli za Utamaduni, Sanaa na Michezo 60 ambapo kati ya hizo 30 zitafanyika nchini Tanzania na nyingine 30 zitafanyika China ambapo wadau wa Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo watapata fursa ya kushiriki na kuonesha kazi zao.

Katika kikao hicho wadau walipata fursa ya kutoa maoni, ushauri,kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ambapo wataalamu wa wizara walitoa ufafanuzi na kujibu hoja zilizowasilishwa na wadau hao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news