Abiria wakutwa na dawa za kulevya Doha

DOHA-Idara ya Forodha ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad jijini Doha, Qatar imefanikiwa kudhibiti na kuzuia jaribio la kuingiza kiwango kikubwa cha dawa za kulevya nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la Penisula,afisa mmoja wa forodha alizima jaribio hilo baada ya kuhisi na kukagua mabegi ya abiria. Afisa huyo alikuta zaidi ya vidonge 3,360 vinavyohusishwa na dawa za kulevya ndani ya mabegi hayo.
Aidha, ripoti ya kukamata ilitolewa na hatua muhimu zilichukuliwa na idara husika kwa haraka. Wakati huo huo, mamlka husika zimesema zitatoa taarifa kamili baada ya uchunguzi wa kina kufanyika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news