DRC yaitunuku Tanzania tuzo ya heshima

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kupitia kwa Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama, Mhe. Peter Kazadi ameikabidhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tuzo ya Heshima (Gardons notre amitié) - inayohusu KUDUMISHA UHUSIANO baina ya Nchi hizo mbili.Tuzo hiyo imepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini DRC, Mhe. Said J Mshana wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyoandaliwa kwa ajili ya Mawaziri wa SADC waliohudhuria Mkutano kuhusu Udhibiti wa Maafa.
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana akiongea jambo baada ya kukabidhiwa Tuzo na Serikali ya DRC.
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana alimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge na Uratibu katika kikao cha Mawaziri wa SADC kilichohusu udhibiti wa maafa kilichofanyika jijini Kinshasa.Hadi kufikia tarehe 25 Mei 2023, Nchi Wanachama sita kati ya kumi na sita zilikuwa zimesaini Mkataba wa Uendeshaji wa Kituo cha Operesheni na Huduma za Kibinadamu cha SADC.
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mawaziri wa SADC uliohusu udhibiti wa maafa uliofanyika jijini Kinshasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news