Waziri Dkt.Tax asisitiza ubora katika kazi kwa watumishi wa wizara

NA MWANDISHI WETU 

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amewasisitiza watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa kujituma na kuzingatia ubora wa kazi wanapotekeleza majukumu yao. 
Waziri Tax ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma tarehe 26 Mei, 2023.

Pia akawaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa wanawajibu wa kuelewa kwa ufasaha bajeti na mipango iliyowekwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 ili kujipanga kutekeleza vipaumbele vya Wizara kikamilifu.
‘’Pamoja na kuielewa mipango ni jukumu lenu pia kupendekeza mipango na mikakati mizuri zaidi katika kutekeleza vipaumbele vya Wizara katika utekelezaji wa majukumu hususan, kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na uwekezaji,” alisema Dkt. Tax.
Kwa upande wa Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Samwel Shelukindo katika hotuba yake ya ufunguzi ameeleza kuwa baraza la wafanyakazi ni takwa la kisheria na pia linaleta fursa ya ushirikishwaji kwa watumishi hasa katika mipango ya uendeshaji wa Wizara na hivyo huchangia ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.
Meza Kuu wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.
Meza Kuu wakishirikiana na Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) kuimba wimbo wa mshikamano daima.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bi. Chiku Kiguhe akifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.

"Hivyo, ni matumani yangu kuwa wajumbe wa mkutano huu mtatoa michango yenye tija ambayo itaboresha Rasimu ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kabla ya kusomwa Bungeni,” alisema Balozi Shelukindo.
Naye Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa, Bw. Samuel Nyungwa akizungumza, ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kuendelea kuthamini umuhimu na tija ya baraza hilo pamoja na kutoa nafasi ya ushirikishwaji wa mipango ya Wizara kwa watumishi.

Lengo la Mkutano wa Baraza la wafanyakazi ni kupitia taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/2023, na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2023/2024, bajeti ambayo inatarajiwa kuwasilishwa Bungeni tarehe 30 Mei 2023. 
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga akifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.

Mkutano huu ulihudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news