JKCI yatangaza kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto

NA DIRMAKINI

WATAALAMU wa magonjwa ya moyo ya watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Mradi wa Little Heart wa Shirika la Mutanda Aid lenye makao yake makuu jijini London nchini Uingereza watafanya kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto kuanzia Mei 12 hadi 19,2023.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 3, 2023 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),Bi.Anna Nkinda.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,kambi hiyo ya siku nane itafanyikia katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
"Tunawaomba wazazi na watu wote wenye watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo hasa wenye matundu ya moyo, matatizo ya mishipa ya damu na valvu za moyo (ASD,PDA,VSD for device closure, PDA an pulmonary valvular stenosis) wawalete katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa ajili ya kufanyiwa uchuguzi na kupata tiba mwafaka,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Pia, taarifa hiyo imesisitiza kuwa, "Tunaendelea kuwaomba wanannchi kuendelea kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa. Mgonjwa mmoja anayefanyiwa upasuaji wa moyo anatumia kati ya chupa sita hadi saba za damu, Hivyo, basi mahitaji ya damu ni makubwa kwa mgonjwa anayefanyiwa upasuaji wa moyo.

"Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa namba 0757843481 Dkt. Jackline Oleyaiti, 0744479506 Dkt.Jimmy France na 0788308999 Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),"imeongeza sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news