NACTVET yafungua dirisha la udahili mwaka wa masomo 2023/2024

NA DIRAMAKINI

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limetangaza rasmi leo Mei 21,2023 kuwa wamefungua dirisha la udahili kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini katika mwaka wa masomo 2023/2024.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Mkurugenzi wa Udhiti, Ufuatiliaji na Tathimini NACTVET,Dkt, Jofrey Oleke amesema, udahili huo wa kozi zote zinazotolewa na vyuo mbalimbali wameufungua rasmi leo Mei 21,2023 hadi Juni 30, 2023 katika awamu ya kwanza.

"Wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na vyuo vyenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kufanya maombi yao kwa umakini ili kupata nafasi ya kujiunga na kozi wanazozipenda.

"Na wote wawe wametimiza sifa na vigezo vya kujiunga na vyuo katika kozi walizoomba kwa mwaka wa masomo 2023/2024 na maombi hayo ya kujiunga yatumwe katika vyuo husika,"ameeleza Dkt.Oleke.

Aidha, Dkt, Oleke aliezea kuwa kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na programu za Afya na Sayansi Shirikishi kwa upande wa Tanzania Bara wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia udahili wa pamoja .

"Kwa wanafunzi wanaopenda kujiunga na kupitia kozi ya Afya na Sayansi Shirikishi hawa wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia udahili wa pamoja yaani Central Admission System-CAS, katika tovuti ya Baraza www.nacte.go.tz

"Baraza pia linawashauri waombaji wote, wazazi na walezi kuhakikisha wanaomba udahili kwenye vyuo ambavyo vimeorodheshwa kwenye muongozo wa udahili kwa mwaka wa masomo 2023/204 ( Admission Guidebook for 2023/204 Academic Year ) ambapo muongozo huo unapatikana katika tovuti ya Baraza ww.nacte.go.tz,"amesema Dkt.Oleke.

Pia, amesema baraza linatoa rai kwa waombaji wote kuandika taarifa zao sahihi pamoja na kutunza taarifa watakazopatiwa na baraza bila kumpatia mtu yeyote ili kuepusha usumbufu katika zoezi zima la maombi yao ya kujiunga na vyuo katika kozi mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news