Papa Francis ateta na CDF mstaafu Jenerali Mabeyo, Mapadre Watanzania

NA DIRAMAKINI

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amekutana na Mapadre Watanzania wanaosoma na kufanya utume wao nchini Italia pamoja na Mkuu wa Majeshi mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo.

Maaskofu wote nchini Tanzania wako katika ziara ya Kichungaji yalipo makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani mjini Vatican tangu Mei 14 hadi Mei 21, 2023.

Kwa mujibu wa tarifa kutoka Kanisa Katoliki nchini,katika ziara hiyo wameambatana na Mapadre kadhaa akiwemo Padre Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Padre Chesco Msaga C.PP.S Naibu Katibu Mkuu (TEC) bila kumsahau Padre Thomas Kiangio Msimamizi wa Jimbo Katoliki Tanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news