Rais Dkt.Mwinyi kushiriki Jukwaa la Kimataifa la Tatu la Uchumi nchini Qatar

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar leo Mei 21, 2023 kuelekea nchini Qatar kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi linalofanyika jijini Doha.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Zanzibar katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,akielekea nhini Qatar, kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Tatu la Uchumi linalofanyika Doha nchini Qatar, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu.(Picha na Ikulu).

Jukwaa hilo linalodhaminiwa na Kampuni ya Kimataifa ya Bloomberg lenye kauli mbiu isemayo “Simulizi za Ukuaji Kimataifa" hufanyika nchini Qatar kila mwaka

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya washiriki ikiwa ni pamoja na viongozi wa kampuni kubwa duniani, viongozi wa juu wa Serikali, na pia mamlaka zinazohusika za Qatar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news