Prof.Muhongo, wanakijiji Nyasaungu wadhamiria jambo kubwa

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo, ametembelea Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifu kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini leo Mei 30,2023.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, Prof. Muhongo ametembelea miradi hiyo inayotekelezwa kijijini hapo ukiwemo ujenzi wa shule ya sekondari na ujenzi wa zahanati, 

Uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule yao ya msingi (S/M Nyasaungu). Aidha, kero zilizotolewa na kupata majibu kutoka kwa Mbunge huyo ni kuhusu upungufu mkubwa kwenye upatikanaji wa maji, umeme chakula (ukame) na walimu wa S/M Nyasaungu. 

Ujenzi wa Nyasaungu Sekondari, 

Kata ya Ifulifu haikuwa na Sekondari yake, na inashukuru Serikali kuchangia kwa kiasi kikubwa sana ujenzi wa Sekondari ya Kata (Ifulifu Sekondari) kijijini Kabegi.
"Kijiji cha Nyasaungu ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu. Kijiji hiki kiko pembezoni na mbali na vijiji vingine vya kata hii. Vilevile, jiografia yake (mito, vichaka, n.k.) inakifanya kuwa na ugumu wa kufikika, hasa wakati wa mvua, mazingira haya ni hatarishi kwa wanafunzi,"imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa. 

"Ujenzi wa Nyasaungu Sekondari umeanza kwa kutumia michango ya wanakijiji, Mbunge wa Jimbo na 
Mfuko wa Jimbo. Pia Halmashauri inaombwa ianze kuchangia ujenzi wa sekondari hii ambayo watumiaji wake wengi watakuwa watoto wa wafugaji wa Kijiji cha Nyasaungu."

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,Nyasaungu Sekondari itafunguliwa Januari 2024 kwani ujenzi umefikia hatua ya kukamilisha vyumba vitatu vya madarasa,choo cha matundu sita na jengo la utawala.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa, Mbunge wa Jimbo ataendelea kuchangia ujenzi huu kama alivyofanya hapo awali. 

"Wanakijiji wameamua kuendelea na ujenzi wa Sekondari yao kuanzia Juni 10, 2023. Wakianza ujenzi tarehe hiyo Mbunge huyo atawachangia saruji na mabati.

"Kwa sasa, Jimbo letu linajenga sekondari nne mpya, ambazo ni Nyasaungu Sekondari, (Kata ya Ifulifu, sekondari ya pili ya Kata) Muhoji Sekondari, (Kata ya Bugwema, sekondari ya pili ya Kata) Wanyere Sekondari (Kata ya Suguti, sekondari ya pili ya Kata) Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba (Kata ya Etaro, sekondari ya pili ya Kata).

"Jimbo letu lenye Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374, lina jumla ya Sekondari 27 (25 za Kata, na 2 za binafsi."
Picha za hapa zinaonesha Kikao cha leo cha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na wananchi wa Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifuli, Musoma Vijijini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. The power of community Engagements to social and development adds value on project monitoring and supervision.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news