Rais Dkt.Samia afanya uhamisho na uteuzi wakuu wa mikoa, wilaya

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya baadhi ya wakuu wa mikoa, uteuzi wa mkuu wa mkoa, uhamisho wa wakuu wa mikoa na uteuzi wa mkuu wa wilaya.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 23, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Mhe. Said Mohamed Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Mhe. Mtanda ni Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoani Tabora. Anachukua nafasi ya Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee. Meja Jenerali Mzee ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Pia, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Mhe. Sendiga ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, anachukua nafasi ya Mhe. Nyerere ambaye amehamishiwa mkoa wa Rukwa.

Aidha, Mhe. Charles Makongoro Nyerere amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Mhe. Nyerere ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, anachukua nafasi ya Mhe. Sendiga ambaye amehamishiwa mkoa wa Manyara.

Wakati huo huo,Mheshimiwa Rais Dkt.Samia memteua Bw. Kenani Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo. Anachukua nafasi ya Mhe. Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.Mabadiliko, uhamisho na uteuzi huu unaanza mara moja.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uapisho wa Mkuu wa Mkoa mpya utafanyika tarehe 24 Mei, 2023 saa 10:00 jioni, Ikulu Chamwino.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news