Waziri Dkt.Tax asisitiza umoja na mshikamano barani Afrika

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ameshiriki maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (katikati) na Balozi wa Visiwa vya Comoro na Mkuu wa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini (kushoto) wakiimba wimbo wa Afrika wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023.

Maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika yalifanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023 na kuhudhuriwa na Jumuiya ya Mabalozi wa nchi za Afrika na Taasisi za Kimataifa za Afrika zilizoko nchini. 

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mhe. Dkt. Tax alitoa rai kwa nchi za Afrika kuungana ili kukua na kuwa na uchumi imara na kuongozwa na misingi na mawazo ya kuunganisha waafrika na hivyo kudumisha amani na usalama na kupata maendeleo ambayo yatatokana na utambulisho wake , urithi wa pamoja, maadili ya pamoja, mitazamo na ubunifu wa watu wake. 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelikindo (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika Bi Ellen Maduhu waliposhiriki hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023

“Afrika lazima ijengwe kwa kuungana ili ishamiri, iwe na uchumi imara na kuongozwa na misingi ya kuunganisha waafrika ili kulinda amani na usalama ambayo maendeleo yake yanatokana na utambulisho wake yenyewe, urithi wa pamoja, maadili ya pamoja, mitazamo na ubunifu wa watu wake,” alisema Mhe. Waziri. 

Dkt. Tax pia amezisihi nchi za Afrka kutumia vizuri fursa za kiuchumi zilizopo ili kwa kuchochea ufanyaji biashara miongoni mwao na kufikia azma ya utekelezaji wa malengo ya Agenda 2063. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023.

Amesema Afrika ni bara la pili kwa ukubwa likiwa na watu zaidi ya bilioni 1.2 na hivyo kuwa na fursa mbalimbali ambazo zikitumiwa vizuri zitawezesha waafrika kufikia azma ya utekelezaji wa Agenda 2063. 

“Bara la Afrika ni la pili kwa ukubwa duniani likiwa na watu zaidi ya bilioni 1.2, tuna fursa nyingi, naomba nichukue fursa hii nisisitize katika kutumia fursa hizo zikiwemo za biashara, naamini kuwa kama sisi wote tutafanya biashara miongoni mwetu tutafanikiwa kutekeleza malengo tuliyojiwekea katika agenda 2063,” alisisitiza. 
Baadhi ya washiriki wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023,

Alisema wakati Afrika inaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake ni muhimu ikaangalia kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “Uharakishaji na Utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika” na kuongeza kuwa Umoja wa Afrika umechukua hatua kwa kushirikiana na taasisi zake na zile za kikanda kuharakisha utekelezaji wa Soko hilo unafanyika kwa manufaa ya waafrika. 

Amesema Soko la Eneo Huru la Bara Afrika (AfCFTA) ni chombo muhimu katika kukuza na kuchochea ufanyaji wa biashara miongoni mwa waafrika na hivyo kukuza maeneo mbalimbali ya uchumi ikiwa ni moja ya mafanikio ya muingiliano wa kiuchumi na maendeleo kwa watu wake 
Bw. Ahmed Salim Ahmed Salim, Mtoto wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika (OAU -(1989-2001) Mhe. Balozi Dkt. Salim Ahmed Salim ) akiangalia tuzo maalum ya Baba yake kabla ya kukabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (katikati) na Balozi wa Visiwa vya Comoro na Mkuu wa Mabalozi wa nchi za Afrika nchini (wa pili kulia) iliyotolewa na Mabalozi wa Nchi za Afrika walioko nchini wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023.

Amesema wakati wananchi wa Afrika wanaangalia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo ni wakati muafaka pia kuangalia changamoto zinazolikabili bara la Afrika ambazo zinazuia kushamiri kwa bara hilo. 

Ametaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni mabadiliko ya serikali yasiyofuata demokrasia, migogoro ya kivita, mabadiliko ya hali ya hewa, umasikini na ukosefu wa ajira na kuongeza kuwa viongozi wa Afrika lazima waunganishe jitihada zao na kuja na mikakati ya pamoja kama njia za kutatua changamoto hizo. 
Balozi wa Visiwa vya Comoro na Mkuu wa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023.

Awali akizungumza katika Maadhimisho hayo Kiongozi wa Mabalozi wa na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini na Mhe. El Badaoui Mohamed Fakih alisema Bara la Afrika linajivunia mafanikio makubwa ambayo limeyapata katika siku za hivi karibuni.

Amesema mafanikio hayo yanatokana na kujipanga na kuanzishwa kwa mifumo wa utendaji kazi katika Umoja wa Afrika ambayo inashughulikia changamoto mbalimbali zitokanazo na matatizo yanayoikumba dunia na kutafuta njia za kukabiliana na matatizo hayo kwa pamoja. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Nchi za Afrika walioko nchini wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023.

Mhe. Balozi El Badaoui alipongeza kitendo cha Serikali kushirikiana na Jumuiya ya Mabalozi wa Afrika waliopo nchini katika kuadhimisha Siku ya Afrika ambayo imefikisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika mwaka 1963. 

Katika hafla hiyo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika (1989-2001) Mhe. Balozi Dkt. Salim Ahmed Salim alitunukiwa tuzo maalum na Umoja wa Mabalozi wa Afrika nchini ambayo ilipokelewa na mtoto wa Dkt. Salim Bw. Ahmed Salim Ahmed kwa niaba ya baba yake. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) (katikati) katika picha ya pamoja na wenza wa Mabalozi wa Nchi za Afrika walioko nchini wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023.

Hafla hiyo ya maadhimisho ya miaka 60 ya Siku ya Afrika iliandaliawa kwa pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Jumuiya ya Mabalozi wa Afrika waliopo nchini

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news