JK ASHIRIKI MKUTANO WA JUKWAA LA 7 LA UONGOZI AFRIKA ACCRA NCHINI GHANA

NA MWANDISHI WETU

RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameungana na Marais wengine Wastaafu wa Afrika kushiriki katika Mkutano wa Jukwaa la 7 la Uongozi Afrika (ALF 2023). Mkutano huo umefanyika katika Jiji la Accra, Ghana miaka minne baada ya kufanyika mara ya mwisho mwaka 2019. 
Mkutano huo umejadili mada mbalimbali ikiwemo "kukuza biashara ya baina ya nchi za Kiafrika ili kufungua fursa zitokanazo na kilimo".

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali umeratibiwa kwa pamoja kati ya Taasisi ya Uongozi ya Tanzania (Uongozi Institute) na Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AFCFTA). 
Rais Kikwete ni Mlezi wa Jukwaa hilo la Uongozi Afrika, alichukua nafasi hiyo kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Tatu wa Tanzania, Hayati Benjamin Mkapa.

Mkutano huo umehudhuriwa na idadi kubwa zaidi ya Viongozi Wastaafu wa Afrika wakiwemo aOlisegun Obasanjo wa Nigeria, Mohamed Moncef Marzouki wa Tunisia, Goodluck Jonathan wa Nigeria, Thomas Bon Yayi wa Benin, Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone, Hailemariam Desalegn wa Ethiopia na Ellen Sirlief Johnson wa Liberia.

Aidha, Katibu Mkuu wa AFCFTA, ambayo ndiyo Taasisi ya Kibara iliyopewa jukumu la kukuza biashara baina ya nchi za Kiafrika na kuongeza kiwango cha biashara ya Afrika katika masoko ya Dunia pia amehudhuria.
Jukwaa la ALF linasifika Duniani kuwa Jukwaa pekee katika Bara la Afrika ambalo linatoa fursa kwa Viongozi Wastaafu wa Nchi na Serikali kujumuika kwa pamoja na kujadiliana kwa uwazi juu ya changamoto mbalimbali zinazolikabidi bara la Afrika. 

Katika mikutano huo Viongozi hupata fursa ya kutoa mapendekezo na ushauri kwa Viongozi wa sasa waliopo madarakani kwa lengo la kuboresha maslahi ya nchi na watu watu wa Afrika.

Kadhalika, miongoni mwa masuala yaliyojitoleza katika majadiliano hayo ni kwa Serikali kuweka mikakati na kufanya jitihada za dhati kutambua nafasi ya vijana wa kiafrika katika kukuza sekta ya kilimo ambayo ndiyo inayotoa ajira nyingi kuliko sekta zote.
Aidha, vikwazo vinavyokwamisha ushiriki wa vijana katika kilimo vilijadiliwa kwa kina, huku Mpango wa Serikali ya Awamu ya Sita nchini Tanzania wa BBT (Build Better Tomorrow) ukisifiwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa na nchi nyingine za kiafrika.

Mpango wa BBT unalenga kumsaidia kijana kupata ardhi, pembejeo na mtaji wa kufanya kilimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news