Waziri Mkuu kukutana na Kamati ya Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, Mawaziri na TRA

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajia kukutana na Kamati ya Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo,mawaziri wa sekta husika na Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA).
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Mei 17, 2023 saa 8 mchana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni Ikulu jijini Dar es Salaam kwa unaratibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, CPA Amos Makala.

"Kwa sasa Serikali inaendelea kuwasihi wafanyabiashara wa soko hilo kuendelea na shughuli zao za biashara wakati Serikali inajiandaa kukutana nao kwa lengo la kuwasikiliza na kushughulikia kero zinazowakabili,"imefafanua sehemu ya taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news