Haya hapa majina ya wateule 91 tuzo za EJAT 2022

ARUSHA-Jopo la majaji saba lililokaa Bagamoyo mkoani Pwani kwa siku tisa kuanzia Juni 10 – 18, 2023, kupitia kazi 893 zilizowasilishwa kwa ajili ya mashindano ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2022, limekamilisha kazi yake kwa kupata wateule 91.

Jopo hilo lilitumia siku tisa badala ya nane kutokana na ongezeko la kazi 295 kutoka kazi 598 za EJAT 2021. Hapa niwapongeze na kuwashukuru majaji kwa kazi kubwa waliyoifanya kupitia kazi hii.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tuzo hizi, waandishi wa habari walituma kazi zao kwa njia ya mtandao hali ambayo imerahisisha kazi kwa majaji na Sekretariati. Baraza litaendelea na utaratibu huo katika Tuzo zijazo.

Safari hii jumla ya waandishi 91 wameteuliwa kati ya waandishi 728 waliowasilisha kazi zao. Kati ya hao, 36 wanaandikia magazeti, 27 mitandao ya kijamii (Online) na 15 kutoka radio wakati wanaotokea kwenye runinga walikuwa 13.

Pia kati ya wateule hao, 44 ni wanawake ambapo 16 ni kutoka kwenye magazeti, 12 kutoka mitandao ya kijamii na sita kutoka radio na runinga ni 10. Wateule wanaume ni 47, ambao 20 wanaandikia magazeti, 10 ni waandishi wa radio na runinga ni saba, ambapo mitandao ya kijamii ilikuwa na waandishi 10.

Katika Tuzo za mwaka juzi yaani EJAT 2020, jumla ya waandishi 59 waliteuliwa kuingia katika hatua hii, ambapo EJAT 2021 waandishi wa habari 60 waliingia katika kinyang’anyiro hicho.

Jopo la Majaji liliongozwa na Mkumbwa Asaad Ally. Majaji wengine ni Mwanzo Lawrance Millinga, Peter Wallace Nyanje, Mbaraka Abdi Islam, Dk, Egbert Emmanuel Mkoko, Rose Haji Mwalimu, na Nasima Haji Chum.

Washindi wa tuzo hizo watajulikana rasmi katika kilele cha Tuzo za EJAT 2022 zitakazofanyika Julai 22, 2023 katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Haki Jinai.

Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT ni Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambalo ni Mwenyekiti, Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Taasisi ya Habari ya Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-Tan), Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), HakiElimu, ANSAF, na SIKIKA.

 Makundi yaliyoshindaniwa ni :

  1. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchumi, Biashara na Fedha;
  2. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Michezo na Utamaduni;
  3. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo na Biashara ya Kilimo;
  4. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu;
  5. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi;
  6. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi;
  7. Tuzo za Uandishi wa Habari za Data;
  8. Tuzo za Uandishi wa Habari za Haki za Binadamu na Watu;
  9. Tuzo za Uandishi wa Habari za Utawala Bora na Uwajibikaji;
  10. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Jinsia na Watoto;
  11. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini;
  12. Tuzo za Uandishi wa Habari za Watu wenye Ulemavu;
  13. Tuzo za Uandishi wa Habari za Afya;
  14. Tuzo ya Uandishi wa Sayansi na Teknolojia;
  15. Tuzo za Uandishi wa Habari za Ushirika;
  16. Tuzo za Uandishi wa Habari za Kodi, Tozo na Mapato;
  17. Tuzo za Uandishi wa Habari za Sensa;
  18. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utunzaji wa Mazingira na vyanzo vya Maji;
  19. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya ya Uzazi
  20. Kundi la Wazi;
Ifuatayo ni orodha ya wateule kutoka vyombo mbalimbali vya habari na mikao yao

SN  JINA LA MTEULE  CHOMBO      MKOA
1    Ephrahim Bahemu      Mwananchi    Dar es Salaam
2   Peter Elias                Mwananchi       Dar es Salaam
3 Shabani Njia Hamisi    Nipashe         Shinyanga
4 Flora Primo Siriwa    Moshi FM      Kilimanjaro
5 Elizabeth Kilindi          Nipashe       Njombe
6 Jackline Silemu          ITV               Dar es Salaam
7 Salumu Vuai Issa       Zanzibar Leo    Zanzibar
8 Rahma Suleiman          Ali Nipashe     Zanzibar
9 Hermina Emil Mkude    Nukta Africa   Dar es Salaam
10 Haji Nassoro Mohammed  Zanzibar Leo   Pemba
11 Anthony Mayunga          Jamhuri            Mara
12 Faraja Benedict Masinde    Gazetini     Dar es Salaam
13 Mohammed Makonda     Radio Kwizera     Kagera
14 Catherine Madabuke      Mazingira FM      Mara
15 Hamisi Makungu Hamisi    Pangani FM      Tanga
16 George Henry Helahela    The Citizen Digital    Dar es Salaam
17 Hazla Omary Quire          TSN digital        Dar es Salaam
18 Julius Mathias Mnganga     Mwananchi     Dar es Salaam
19 Mussa Juma Siwayombe     Mwananchi    Arusha
20 Ramadhani Kabanga Mvungi   Azam TV    Arusha
21 Naishooki Alais Makeseni       Star TV    Dodoma
22 Issa Juma Ramadhani          Dar24          Dar es Salaam
23 Elizabeth Edward Kusekwa     Mwananchi    Dar es Salaam
24 Warioba Igombe Warioba        Uhuru         Morogoro
25 Vumilia Alex Macha         Savvy FM          Arusha
26 Tumaini Godwin Msowoya     Mwananchi     Iringa
27 Imani Henrick Luvanga          Kings FM      Njombe
28 Nicolaus King Mwanalus       Wasafi TV   Dar es Salaam
29 Vicky Ebeneza Kimaro    Habari Leo       Dar es Salaam
30 Ezekiel Hassan Shamakala       TBC Taifa     Dar es Salaam
31 Omary Hussein Omary     Star TV     Morogoro
32 Khamisuu Abdallah Ali    Zanzibar Leo       Zanzibar
33 Mukrim Mohamed Khamis      KTV TZ Online   Zanzibar
34 Haika Kimaro                Habitat News            Mtwara
35 Adella H. Tillya             Wasafi FM        Dar es Salaam
36 Harith Jaha Ally           Watetezi TV        Mwanza
37 Alex Selestine Kazenga         Jamhuri      Dar es Salaam
38 Imani Raphael Makongoro       Mwananchi    Dar es Salaam
39 Najjat Haji Omar                     The Chanzo        Zanzibar
40 Lukelo Francis Haule             The Chanzo     Dar es Salaam
41 Saddam Sadick Mayala       Mwanasport      Dar es Salaam
42 Fatuma Mtemangani          Radio Ulanga FM     Dar es Salaam
43 Josephine Sebastian        The Citizen          Mwanza
44 Manyerere J. Nyerere           Jamhuri           Dar es Salaam
45 Albuni Albuni Mwedadi        Mlimani Radio      Dar es Salaam
46 Lucy Patrick Samson          Nukta Africa          Dar es Salaam
47 Juma Mussa Issihaka           Mwananchi      Dar es Salaam
48 Warioba Igombe Warioba         Uhuru         Morogoro
49 Yusra Said Shaaban        RSV Online TV       Zanzibar
50 Protte Profit Mmanga         Leo TV online      Arusha
51 Amina Salum Kasheba           Uhuru     Dar es Salaam
52 Joseph Kirati Kirati         The Chanzo     Dar es Salaam
53 Alfred Lasteck Mushi         BBC Swahili     Dar es Salaam
54 Mariam Shaban Mbwana       Mwananchi     Dar es Salaam
55 Heneliko Leonard Malo             Bomba FM    Iringa
56 Kelvin Paul Matandiko          Mwananchi   Dar es Salaam
57 Abel Claud Kilumbu           Dar24        Dar es Salaam
58 Mwajuma Hassan Rajab           EATV      Dar es Salaam
59 Jackline Victor Kuwanda          The Chanzo     Dar es Salaam
60 Herieth Makwetta              Mwananchi      Dar es Salaam
61 Sanula Athanas                        Nipashe      Dar es Salaam
62 Daniel Mwalubuli Nukta               Africa     Dar es Salaam
63 Pamela Nesphory Chilongola         Mwananchi     Dar es Salaam
64 Khadija Ali Yusuph                    Radio Jamii Mkoani   Zanzibar
65 Cosmas C. Mwamposa            Pangani FM        Tanga
66 Francis Dhamira Kajubi               The Guardian     Dar es Salaam
67 Asifiwe Brown Mbembela                The Chanzo Mbeya
68 Janet Kimario Joseph           Mwananchi       Kilimanjaro
69 Said Ally Sindo                Storm FM       Geita
70 Ayoub Stanley Nyondo             Shamba FM            Iringa
71 Anna Peter Mbuthu                  TBC1       Dar es Salaam
72 Daniel Hezron Limbe              Malundeblog      Geita
73 Stanslaus Bernard Lambart        Dar24      Dar es Salaam
74 Zuhura Hassan Makuka              Dar24      Dodoma
75 Anna Thadei Augustino                  EATV      Arusha
76 D’jaro Deus Arungu        TBC FM      Dar es Salaam
77 Baraka Mnyalei Loshilaa       Mwananchi     Dar es Salaam
78 Festo Charles Lumwe          Dar24       Dar es Salaam
79 Peter Lugendo John          TBC Taifa       Dar es Salaam
80 Dafrosa Prosper Ngailo             Azam TV    Dar es Salaam
81 Zuhura Juma Said              Zanzibar Leo       Zanzibar
82 Elesia Thomas Haule       Azam TV      Dar es Salaam
83 Suleiman Omary Mwiru         Nukta Africa    Dar es Salaam
84 Adam Gabriel Hhando            CG FM   Tabora
85 Grace Elibariki Mbise     Star TV       Mwanza
86 Ahmadi Ally Mramba        TBC1     Dodoma
87 Heldina G. Mwingira        Dar24     Dar es Salaam
88 Augusta Mathias Njoji        Nipashe      Dodoma
89 Clezencia Tryphone              Mwanasport Dar es Salaam
90 Dauka Abraham Somba              Dar24  Dar es Salaam
91 James Daud Lerombo               TBC1     Mwanza

Kajubi D. Mukajanga
Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi EJAT 2022

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news