Tanzania yaishukuru UK Export Finance kwa kuunga mkono miradi ya maendeleo Zanzibar

NA BENNY MWAIPAJA-WFM

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameishukuru Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF), kwa kukamilisha mchakato wa utoaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani humo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati kikao na ujumbe kutoka Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Bw. Tim Reid, ambapo aliwashukuru kwa kukamilisha mchakato wa utoaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani humo. Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Treasury Square, jijini Dodoma.

Dkt. Nchemba ametoa pongezi hizo jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa UK Export Finance (UKEF), aliyepo nchini kwa ziara ya kikazi.

Alisema kuwa miradi hiyo, si tu kwamba itachokea shughuli za kiuchumi za visiwa hivyo ukiwemo utalii, bali pia itaboresha maisha ya wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

Dkt. Nchemba aliiomba taasisi hiyo, kuangalia uwezekano wa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kipande cha tano na sita cha reli ya kisasa kinachoanzia Isaka hadi Mwanza chenye urefu wa kilometa 249 na mradi wa maji wa Bwawa la Farkwa kwa ajili ya kuondoa changamoto ya uhaba wa maji katika Jiji la Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya UK Export Finance Bw. Tim Reid, akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ambapo aliihakikishia Tanzania kupata fedha kwa ajili ya miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani humo, lakini pia kuendelea kufadhili miradi mingine ya kimkakati itakayowasilishwa na Serikali ikiwemo maji na nishati. Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Treasury Square, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, (kushoto), Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Justine (katikati) na Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Rished Bade (Kulia), wakisikiliza jambo wakati wa kikao na ujumbe kutoka Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw. Tim Reid, ambapo aliwashukuru kwa kukamilisha mchakato wa utoaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani humo. Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Treasury Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisikiliza jambo kutoka kwa ujumbe wa Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw. Tim Reid, ambapo aliwashukuru kwa kukamilisha mchakato wa utoaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani humo. Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Treasury Square, jijini Dodoma.

Alisema kuwa Mradi wa reli ya kisasa unaombewa ufadhili wa kipande cha Isaka hadi Mwanza ambao taratibu zake za ununuzi zimekamilika na mkandarasi amepatikana pamoja na kipande cha reli cha kuanzia Kaliua hadi Kalemi kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo ambao uko katika hatua za ununuzi, utafungua biashara katika ukanda huo na kuchochea uchumi na maendeleo ya watu.

Dkt. Nchemba aliiomba Taasisi hiyo kuitafutia Tanzania wawekezaji watakao wekeza katika miradi mbalimbali ya uzalishaji ukiwemo mradi wa barabara ya kulipia ya Chalinze hadi Morogoro ambayo baadae imekusudiwa kufika hadi Dodoma.
Ujumbe kutoka Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF) ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya UK Export Finance Bw. Tim Reid (kulia), Mkuu wa Masuala ya Biashara Bw. Vomic Nur Shah (katikati) na Mkuu wa masuala ya Fedha ukanda wa Afrika Mashariki Bw. Isaac Kahara (kushoto), wakisikiliza jambo wakati wa kikao na ujumbe wa Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ambapo ujumbe huo kutoka UKEF uliihakikishia Tanzania kupata fedha kwa ajili ya miradi ya kimkakati itakayowasilishwa na Serikali ikiwemo maji na nishati. Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Treasury Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya UK Export Finance Bw. Tim Reid, baada ya kikao chao, ambapo aliwashukuru kwa kukamilisha mchakato wa utoaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na ujenzi wa miundombinu ya barabara visiwani humo. Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Treasury Square, jijini Dodoma.

Alisema kuwa miradi hiyo ni mkakati wa Serikali, ikiongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wenye lengo la kukuza ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa UK Export Finance (UKEF), Bw. Tim Reid, aliihakikishia Tanzania kupata fedha kwa ajili ya miradi hiyo lakini pia kuendelea kufadhili miradi mingine ya kimkakati itakayowasilishwa na Serikali ikiwemo maji na nishati.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Taasisi ya Uingereza inayohusika na utoaji mikopo ya UK Export Finance (UKEF), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw. Tim Reid (wa nne kushoto) ,ambapo walizungumza mambo mbalimbali ikiwemo kupata mikopo kwa ajili ya miradi ya kimkakati ikiwemo uwanja wa ndege, barabara, maji na nishati, Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Treasury Square, jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, (wanne kulia), Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Justine (wa tatu kulia) na Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Rished Bade (wa pili kulia), Kamishna wa Idara ya Mipango ya Kitaifa - Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Mursali Milanzi, Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Madeni - Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Tiba Kisonga (wa kwanza kushoto), Mkuu wa masuala ya Fedha ukanda wa Afrika Mashariki – UKEF Bw. Isaac Kahara (wa pili kushoto), na Mkuu wa Masuala ya Biashara - UKEF Bw. Vomic Nur Shah (wa tatu kushoto).

Alisema kuwa, taasisi hiyo imekamilisha mchakato wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara Visiwani Zanzibar na kwamba fedha hizo zitatolewa mara tu baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kimkataba.

Uk Exporter Finance ni Wakala wa Serikali ya Uingereza inayojihusisha na kusaidia uagizaji na uingizaji wa bidhaa nchini humo kwa kutoa mikopo ya mitaji na kukatia bima bidhaa hizo lakini pia kuhakikisha kuwa zinakuwa na bei shindani kwenye masoko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news