Waziri Mhandisi Masauni:Maboresho makubwa yatafanyika Jeshi la Polisi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameweka wazi baadhi ya maeneo ambayo wizara imepanga kuyafanyia maboresho makubwa ili kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wananchi kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwasilisha maoni kuhusu mambo mbalimbali mbele ya wajumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai,tume hiyo imeundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuangalia namna ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande.Kikao hicho kimefanyika Juni 6,2023 jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Ameeleza hatua hiyo baada ya kumaliza kutoa maoni kwa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai inayoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande huku vyombo vilivyopo chini ya wizara yake ni miongoni mwa taasisi ambazo tume hiyo inafanyia kazi pia katika uboreshaji huo,Tume hiyo iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan lengo ikiwa kupitia taasisi na mifumo mbalimbali inayoshughulika na utoaji haki.

“Tunatimiza azima ya Amiri Jeshi Mkuu,Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo ametaka kuona maboresho katika vyombo vya utoaji haki,hasa mambo yanayosababisha malalamiko kutoka kwa wananchi ambayo yamekua kero na yanaathiri haki za wananchi, kwahiyo maoni yangu niliyotoa yamelenga Zaidi kuleta mabadiliko ya kimuundo,kisheria na kikanuni na kuweza kuwa kuwa na vyombo vya polisi,magereza ambavyo havitakuwa na changamoto katika maeneo ya utendaji kazi.

“Maeneo ambayo nimetoa maoni na kama wizara tumedhamiria kuyaboresha ni eneo la Upelelezi,Ubambikizaji wa Kesi,Utoaji wa Dhamana na Mrundikano wa Mahabusu katika Vituo vya Polisi na Magereza, hayo yamekua maeneo ambayo tumekua tukipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi,”ameongeza Waziri Mhandisi Masauni.

Katika kikao hicho, Waziri Mhandisi Masauni pia alipata wasaa wa kubadilishana mawazo na wajumbe mbalimbali wa tume hiyo,wakiwemo Wakuu wa Jeshi la Polisi Wastaafu, Said Mwema na Balozi Ernest Mangu huku tume hiyo ikitarajiwa kukamilisha ukusanyaji wa maoni ifikapo mwezi Aprili, mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news