Wahamasishwa kujitokeza kupata mafunzo ya filamu

NA ELEUTERI MANGI-WUM

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Saidi Yakubu ametoa wito kwa vijana pamoja na watu wenye hamasa kujifunza kazi ya filamu nchini wajitokeze kupata mafunzo ya filamu wanayotolewa na Maltichoice Tanzania ambayo ni fursa adimu ya kuongeza ujuzi, uzoefu na maarifa yao kwenye kazi hiyo.
Akizungumzia ukuaji wa Sekta ya Filamu nchini, Katibu Mkuu, Bw. Yakubu amesema kuwa nafunzi sekta ya filamu nchini inakua kwa kasi ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita kwa mwaka uzalishaji wa filamu nchini uklikuwa ni filamu 200 ambapo kwa sasa zinazalishwa filamu 2000 kwa mwaka ikizingatiwa soko la filamu linakua sana ndani na nje ya Tanzania.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema hayo Juni 23, 2023 jijini Dar es salaam alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa dirisha la maombi kwa ajili ya msimu wa tano wa mafunzo mafunzo maalum ya umahiri ya mwaka mmoja.

“Sasa hivi Tanzania tuna mcheza filamu namba moja ambaye filamu yake inazungumzia utalii, Mhe, Rais Dkt. Samia Suluhiu Hassan kwenye filamu ya The Royal Tour sasa hivi mtaiona inachezwa pia kwenye ndege za Air Tanzania Pamoja na ndege nyingine inasaidia sana na matunda yake yameanza kuonekana katika kutangaza utalii nan chi kwa ujumla,” amesema Katibu Mkuu Bw. Yakubu.

Aidha, ameipongeza Multichoice Tanzania kwa kazi nzuri ya kuleta mapinduzi katika uzalishaji wa filamu Tanzania na barani Afrika kwa kutoa mafunzo ya umahiri kwa vijana wenye kipaji katika uwanda huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Jacquiline Woiso amesema wanazindua msimu wa tano wa mafunzo hayo ambapo Tanzania ina nafasi ya kupeleka wanafunzi watano watakaojumuika na wenzao kutoka Ethiopia, Kenya na Uganda katika kituo cha mafunzo cha Nairobi mwaka 2024.

Hadi sasa Tanzania ina jumla ya wanufaika 18 na wahitimu waliotangulia wameonyesha mafanikio makubwa kazi zao zimepokea tuzo mbalimbali za filamu kutoka katika matamasha makubwa ndani na nje ya Tanzania ambapo mwaka 2022, filamu ya "Still Okay To Date" ya mhitimu wa darasa la 2020, Kefa Igilo, ilishinda tuzo tatu katika Tamasha la Tanzania Filam na ilishinda pia Tuzo ya Filamu Bora Afrika Mashariki katika tamasha kubwa la filamu la Kalasha nchini Kenya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news