Waziri Dkt.Tax afanya ziara Chuo cha Diplomasia Indonesia

JAKARTA-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akiwa anaendelea na ziara yake nchini Indonesia, ametembelea Chuo cha Diplomasia cha Indonesia.Waziri Dkt.Tax pamoja na ujumbe wake wamepokelewa chuoni hapo na Mkuu wa chuo, Bw.Mohammad Koba

Kufuatia ziara hiyo, Tanzania na Indonesia zimekubaliana kuanzisha ushirikiano baina ya Vyuo vya Kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa chuo na programu za mafunzo kwa Wanadiplomasia, na kubadilishama ujuzi kwa walimu na wanafunzi wa vyuo hivyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news