Hongereni sana-Rais Dkt.Mwinyi

DAR ES SALAAM-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewapongeza wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) na kampuni tanzu Imara Horizon kwa fikra sahihi za uwekezaji wa jengo la Benjamin William Mkapa Health Plaza.

Rais Dkt.Mwinyi ambaye pia ni Msarifu wa taasisi hiyo amesema, kwa hatua ya uwekezaji wa jengo hilo ambalo litakuwa linatoa huduma za afya na ofisi kwa mashirika ya afya ni kielelezo kimojawapo cha mafanikio na kutimiza maono ya kumuenzi Hayati Benjamin William Mkapa.

Ameyasema hayo Julai 27,2023 katika hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Benjamin William Mkapa Health Plaza lililopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Pia, Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendeleza jitihada za kuongeza uwekezaji katika sekta ya afya hususani katika ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa vifaa tiba na upatikanaji wa watumishi wa sekta ya afya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news