Mandonga,Kiduku wadundwa huko Mwanza

MWANZA-Kwa mara nyingine tena, Bondia Mtanzania Karim Mandonga (Mtu Kazi) amepigwa na Bondia wa Uganda, Moses Golola kwa Technical Knock Out raundi ya tatu katika pambano lililochezwa jijini Mwanza.

Mandonga amepigwa TKO ikiwa ni ndani ya siku chache baada ya Julai 22, 2023 kupigwa na Bondia Daniel Wanyoni wa Kenya.

Wakati huo huo, Bondia Mtanzania Twaha Kiduku amepoteza pambano la Ubingwa wa WBF Intercontinental (Ubingwa wa Mabara) dhidi ya Bondia wa Afrika Kusini Asemahle Wellem kwa point katika pambano la raundi 12 lililochezwa jijini Mwanza.

Pambano hilo la uzito wa super middleweight limemfanya Bondia Asemahle kucheza pambano lake la saba bila kupoteza wakati Twaha Kiduku mara ya mwisho kupoteza pambano lolote ilikuwa Mei 20,2021 dhidi ya Bek Nurmaganbet raia wa Kazakhstan.

Pambano hilo la raundi 12 ilishuhudiwa Twaha Kiduku akipoteza kwa pointi za majaji wote watatu huku Asemahle akibeba pointi nyingi baada ya kutawala pambano hilo kwa kiasi kikubwa katika raundi zote 12.

Aidha,Twaha Kiduku mara zote alikuwa anaonekana kumuwinda mpinzani wake ili kumpiga ngumi za ushindi kwenye kona za ulingo.

Ingawa ngumi hizo hazikufanikiwa kwa kiasi kikubwa mbele ya bondia huyo kutoka Afrika Kusini ambaye mara zote alitumia mbinu za kukumbatia pindi anapowekwa kwenye kona za ulingo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news