Tambua thamani ya Ufalme wa Mungu

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa, neno la Mungu katika Jumapili ya 17 ya Mwaka A wa Liturjia ya Kanisa linasisitiza kuupa thamani Ufalme wa Mungu, kama kitu cha kwanza katika maisha ya mwanadamu.

Hayo yamehubiriwa na Padri Alex Maya lleo Julai 30, 2023, anayefanya utume wake katika Parokia ya Ihalu, ambapo alisalisha misa hiyo katika Kanisa la Bikira Maria, Malkia wa Wamisionari, Parokia ya Malya, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.

“Ufalme wa Mungu unafanana na kokolo, ambalo kazi yake ni kuvua samaki wa kila aina, hata hapa dunia wapo watu wa kila aina, wasengenyaji, wazinzi, waongo, wapo wabishi, wote hao wameandaliwa kuutafuta Ufalne wa Mungu.

"Mungu anatupatia mvua ulimwegu mzima, wenye wema na wabaya na hata dhambi zetu hazionekani, je kama tungekuwa na kioo cha kuonesha dhambi zetu ingekuwaje?.

"Mtu ukipita watu wangeona dhambi zako. Jamani tutambue kuwa sote tumeitwa katika Ufalme wa Mungu. Kwa mfano wa kokolo, Je? Wewe ni samaki wa aina gani? Sato, Sangara au wewe ni Kamabale? Samaki Kambale kuanzia baba, mama na watoto wote wana ndevu.”

Padri Maya amesema kuwa, Mtume Paulo alivyoandika kwa Warumi alisema kuwa, Mungu anafanya kazi na wale wampendao, wale walioitwa kwa kusudi lake, mimi na wewe tumeitwa kwa kusudi na Mwenyezi Mungu.

Aliongeza kuwa neno la Mungu linasema,“Siyo sisi tuliyomchagua, bali yeye ndiye alituchagua sisi, kama umechaguliwa na Mungu, je unaitambua thamani hiyo ya kuchaguliwa?.

"Katika azimisho la misa hii, tuombe Mungu atusaidie kila muumini atambue thamani ya Ufalme wa Mbinguni katika maisha yake, Ufalme wa Mbinguni ndiyo kitu cha kwanza na Mungu ndiye anapaswa kuwa kipao mbele cha maisha ya kila mwanadamu.”

Misa hiyo pia ilikuwa na nia na maombi kadhaa ikiwamo kuwaombea marehemu.Tamati ya misa hiyo kulifanyika mchango kwa kumtegemeza mwalimu wa kwaya ambapo katika misa ya kwanza zilipatikana shilingi laki nne na ushehe.

Hadi misa hiyo ya kwanza iliyoanza saa kumi na mbili ya asubuhi inakamilika, hali ya hewa ya eneo la Malya na viunga vyake limekuwa na baridi kali wakati wa usiku na asubuhi, huku mchana jua kali likiwaka, nayo hali ya kijani kibichi imepotea, miti mikubwa ikipukutisha majani yake, huku miti michache inayostahamili ukame pekee ikibakiza majani yake mabichi yasiyo na chanikiwiti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news