Naibu Waziri Nderiananga awashirikisha jambo wanafunzi

KILIMANJARO-Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe.Ummy Nderiananga awaasa vijana kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili kuyafikia malengo waliyonayo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Weruweru alipowatembelea Julai 16, 2023 ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa shule hiyo aliyosoma.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Weruweru alipotembelea mapema Julai 16, 2023 shuleni hapo kwa lengo la kuwapa hamasa wanafunzi wa shule hiyo ambayo aliwahi kusoma na kutoa zawadi za taulo za kike na mafuta ya ngozi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa uongozi wa shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Weruweru wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga (hayupo pichani) wakati alipotembelea shuleni hapo.

Mhe. Nderiananga aliwaeleza upo umuhimu wa kuendelea kuchukua tahadhari za masuala yanayohusu Virusi vya UKIMWI kwani kwa mujibu wa tafiti za viashiria vya VVU na UKIMIWI mwaka 2016/17 zinaonesha kuwa asilimia kubwa ya maambukizi ipo kwa vijana mwenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 hivyo ipo haja ya kuendelea kuwa makini.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Crispin Musiba akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Alitumia fursa hiyo kuwahimiza kujikinga na mimba za utotoni na kutokatishwa tamaa juu ya ndoto zao.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shule ya sekondari ya Weruweru mara baada ya kuwasili shuleni hapo.

"Katika maisha kukatishwa tamaa kupo, lakini kuwa imara hadi wakatisha tamaa wakate tamaa wenyewe, hivyo wanafunzi wa Weruweru muwe imara, majasiri na hakika jitihada zenu hazitapotea bure,"alisema.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga akisalimiana na walimu wa shule ya sekondari ya Weruweru mara baada ya kuwasili shuleni hapo.

Sambamba na hilo aliwatoa wasiwasi wanafunzi wa kidato cha sita kuhusu kuendelea na elimu ya juu kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetenga bajeti ya kutosha katika sekta ya elimu kwa ajili ya kuwawezesha mikopo ya Elimu ya juu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga akiwapakulia chakula wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari ya Weruweru ikiwa ni sadaka yake kwa kuwahudumia na kuwapa zawadi, mara baada ya kutambua mchango wa shule hiyo katika maisha yake.

"Jukumu lenu kubwa ni kuongeza bidii, nidhamu na weledi katika masomo yenu ili kupata fursa ya kuendelea na masoma ya elimu ya juu kisha kuzifikia ndoto mlizo nazo," alisisitiza Mhe Nderiananga
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mwitikio wa Taifa TACAIDS Bi. Audrey Njelekela akiwasilisha mada kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Weruweru wakati wa ziara ya Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu( SBU) Mhe.Ummy Nderiananga shuleni hapo.

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mwitikio wa Taifa TACAIDS Bi.Audrey Ngelekela aliwakumbusha kuendelea kuwa makini kujiepusha na mitandao ya ngono pamoja na kuchukua tahadhari ili kujiepusha na maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga akifurahi na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Weruweru mara baada ya kuzungumza nao.

Alieleza kuwa, Serikali kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa jamii hasa vijana ambao ndio kundi linaloathiriwa zaidi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa mujibu wa takwimu za utafiti wa mwaka 2016/17.
Mratibu wa UKIMWI wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Dkt. Didas Constantine akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa kupima VVU kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Weruweru.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU NA TACAIDS).

Naye Mratibu wa UKIMWI wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Dkt. Didas Constantine aliwakumbusha wanafunzi umuhimu wa kupima afya zao kwa lengo la kujua hali zao za maambukizi iwapo unagundulika kuwa maambukizi inashauriwa kuanza dawa mapema.

Awali akizungumza kuhusu shule ya Weruweru mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi.Rozalia Frimin alimshukuru Naibu waziri kwa ziara yake shule hapo pamoja na kuwapa zawadi ya taulo za kike pamoja na mafuta kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi ikiwa ni sehemu ya shukrani yake kwa mchango wa shule hiyo katika maisha yake.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Weruweru Bi.Rozalia Frimin akizungumza na kuelezea historia ya shule hiyo wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Ummy Nderiananga shuleni hapo.

"Mhe Naibu Waziri tunakushukuru kututembelea leo, hii imetupa hamasa zaidi sisi na wanafunzi wetu kwa kuwa umetambua mchango wa shule ya Weruweru, sisi tutaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuzalisha vijana wasomi na wenye maadili mazuri nchini," alisema Mwalimu Frimin.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news