OUT yazidi kuonesha ufanisi wake Maonesho ya 18 ya TCU

DAR ES SALAAM-Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), kimeendelea kufanya vyema katika maonyesho ya kumi na nane ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia kutokana na uwepo wa kozi hitaji na huduma zilizo bora.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Utafiti wa chuo hiki, Prof. Emmanuel Mhache, wakati wa maonyesho hayo yanayoendelea kurindima katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 17 hadi Julai 22, 2023.
“Ukiangalia wageni wanaotutembelea wengi wamekuja moja kwa moja kufuata chuo hiki ni dalili njema lakini pia uwepo wa kozi ya Msingi umeonekana kuwa ni kivutio kikubwa sana kwa wahitimu wa kidato cha sita na stashahada,"amebainisha Prof. Mhache.
Aidha, Wativa mbalimbali kutoka chuo hiki Julai 20, 2023 wametembelea banda la maonyesho la chuo hiki katika viwanja hivyo vya Mnazi Mmoja kujionea mambo mbalimbali yanayoendelea katika banda hilo.
Akizungumza katika banda hilo, Mtiva wa kitivo cha Elimu, Dr. Shavega, amesema amevutiwa na namna banda lilivyo na watumishi walivyochangamka katika kuhudumia wateja wanaotembelea banda hili.
“Kwa muda mfupi nimeona pamekuwa na wateja wengi hapa lakini pia nimevutiwa na ufanyaji wa udahili wa moja kwa moja hapa bandani unaofanywa na watumishi wetu katika kusaidia wananchi wanaofika kuulizia mambo mbalimbali na kuhitaji kujiunga na chuo hiki wakati huo."
Maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yanayoratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanafanyika kwa mara ya kumi na nane katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ambapo kwa mwaka huu yameanza Julai 17 na yanatarajiwa kumalizika Julai 22, 2023. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kinashiriki kwenye maonesho yanayokutanisha vyuo vikuu na taasisi zote zilizo chini ya tume hiyo, nyote mnakaribishwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news