Rais Dkt.Mwinyi:Zanzibar ipo tayari kupokea mabadiliko ya kiteknolojia

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali imejiandaa kuhakikisha Zanzibar inakuwa mstari wa mbele kuyapokea mabadiliko ya teknolojia ambayo ni msingi muhimu kwa kukuza na kuendeleza uchumi wa kisasa pamoja na kurahisisha maisha ya wananchi wa hali zote.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizindua Mkakati wa Kidigitali wa Serikali na Mfumo wa Bajeti na Matumizi Serikalini, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja jijini Zanzibar leo Julai 29,2023. Kushoto kwa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe.Haroun Ali Suleiman na Mkurugenzi Mtendaji wa e-Government Zanzibar (e-GAZ ), Said Seif Said. Kulia kwa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe.Dkt.Saada Mkuya Salum.(Picha na Ikulu).

Ameyasema hayo leo Julai 29,2023 katika hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Kidijitali wa Serikali na Mfumo wa Bajeti na Matumizi Serikalini (BAMAS) uliyofanyika Hoteli ya Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dkt.Mwinyi amesema, matumizi ya mifumo ya TEHAMA yataleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika utendaji kazi wa Serikali kwa ulazima wa kutumia mifumo hiyo kwa kuwa matumizi ya TEHAMA.

Pia, yataimarisha ukusanyaji wa mapato, kurahishisha utoaji wa huduma sekta ya Afya, Elimu, kudhibiti matumizi ya fedha za umma, kukomesha vitendo vya wizi, kuzuia rushwa na ubadhirifu pamoja na kuimairisha usalama wa nchi.

Aidha, Mheshimiwa Rais amesema, mfumo wa BAMAS unaleta uwazi kwenye matumizi serikalini, utaimarisha uwajibikaji kwa watendaji wa Serikali, kuwezesha mifumo yote ya malipo na matumizi ya fedha za Serikali kusomana kwa haraka na kwa ufanisi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news