Yanga SC yampiga bei Yanick Litombo Bangala

DAR ES SALAAM-Uongozi wa Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam umetangaza kuwa umefikia makubaliano na Azam FC juu ya uhamisho wa mchezaji Yanick Litombo Bangala raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Bangala alijiunga na Yanga mwaka 2021 na amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Yanga kilichosaidia kutwaa mataji mbalimbali ya Ligi Kuu mara mbili.

Sambamba na ASFC mara mbili, kucheza fainali ya CAF na na kuibuka na tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu msimu wa 2021/2022.

Aidha, Bangala ameuzwa kwenda Azam FC kwa ada ya uhamisho ambayo ni siri ingawa tetesi zinasema ni karibu dola 50,000

Mbali na hayo, kwenda kwake Azam FC kunamuweka shakani Issah Ndala raia wa Nigeria ambaye huenda akakatwa ili kufanya idadi ya wachezaji wa kigeni kubaki 12 tu.

‘’Uongozi wa Young Africans SC unapenda kuutarifu umma kuwa tumefikia makubaliano na Klabu ya Azam FC ya kumnunua mchezaji wetu Yannick Bangala.’

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news