Rais Dkt.Samia atengua uteuzi wa wakuu wa wilaya, ateua wapya

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Juni 2, 2023 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa wilaya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Mheshimiwa Mwanahamisi Athumani Munkunda na kumteua Mobhare Holmes Matinyi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi,Mheshimiwa Abel Yeji Busalama. Aidha, amemuhamisha kituo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Mheshimiwa Hashim Shaban Mgandilwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua James Wilbert Kaji kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini mkoani Tanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news