Wanufaika TASAF Kibaha waifurahisha Serikali

NA VERONICA MWAFISI 

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema moja kati ya mbinu ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza kwa wananchi wote ni kushiriki katika kubuni mbinu mbalimbali zitakazowawezesha wananchi kujimudu na kuendesha maisha yao pasipokuwa na changamoto yoyote. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitazama miti ya mbogamboga katika shamba darasa la kilimo cha kisasa kinachotekelezwa na kikundi cha walengwa wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF. 

Mhe. Kikwete ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Janga, Mtaa wa Mwembebaraza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Mhe. Kikwete amesema kuwa, Rais Dkt. Samia amekuwa akitoa fedha nyingi ili ziweze kutumika kupitia mbinu na ubunifu mkubwa wenye ubora ili kuweza kuwainua wananchi kiuchumi. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Janga, Mtaa wa Mwembebaraza katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Mhe. Kikwete ametoa pongezi kwa wananchi na watendaji wakiwemo viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa kuhakikisha utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya miradi ya TASAF inatekelezeka kupitia kilimo cha kisasa.
Muonekano wa kilimo cha kisasa cha nyanya kinachotekelezwa na kikundi cha walengwa wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Sehemu ya wananchi na walengwa wa TASAF wa Kata ya Janga, Mtaa wa Mwembebaraza, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza nao alipokuwa kwenye ziara ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Mhe. Kikwete amesema tangu aanze ziara za kikazi katika baadhi ya mikoa amekuwa akikutana na shuhuda na bunifu wa vitu mbalimbali hivyo ni dhahiri kuwa wananchi na walengwa wa TASAF wamekuwa wakifaidika kupitia bunifu za vitu mbalimbali. 
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon amesema wananchi wa taifa la Tanzania ni watu wenye ukarimu hivyo ni vizuri wakaendelea kushirikiana kwa kuwainua walio chini na kupitia mradi wa TASAF jambo ambalo linatekelezeka kwa asilimia kubwa. 

Naye, Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Bi. Sijaona Muhunzi amesema katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wanatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ajira za muda, mradi wa kuweka akiba na kukuza. 
Sehemu ya watumishi wa Mkoa wa Pwani katika Halmashauri ya Wilaya Kibaha wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.

Katika hatua nyingine, Mhe. Naibu waziri Kikwete amefanya kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Kibaha ambapo amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kujiwekea malengo ya utendaji kazi ili kuboresha kazi zao kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akipokea salamu kutoka kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha wakati wa ziara ya Kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete anaendelea na ziara ya kikazi ya wiki moja katika Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao pamoja na kukagua utekelezaji wa Miradi ya TASAF.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news