Waziri Ummy akaribisha ujenzi hospitali ya watoto

HYDERABAD-Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu ametoa wito kwa Uongozi wa Hospitali ya Watoto ya Rainbow kuwekeza nchini Tanzania ili kuongeza huduma za kibingwa za magonjwa ya watoto nchini.
Waziri Ummy amesema hayo mjini Hyderabad nchini India alipofanya mazungumzo na uongozi huo katika kuimarisha ushirikiano ya huduma za kibingwa za magonjwa ya watoto nchini.

Aidha, Waziri Ummy ameuomba Uongozi huo kuanzisha huduma za PICU (Paediatric Intensive Care Unit) na NICU (Neonatal Intensive Care Unit) katika kila hospitali ya wilaya au Halmashauri ili huduma hii ya watoto ipatikane kwa urahisi kwa wananchi.
Waziri Ummy amesema kuwa, katika kuimarisha ushirikiano na Taasisi hii ambayo ni maalumu kwa ajii ya kutoa huduma za watoto nchini India, serikali itaandaa hati ya mashirikiano (MoU) yenye lengo la kuimarisha huduma za kibingwa za watoto nchini.
Hata hivyo, Uongozi wa Hospitali ya Rainbow umeahidi kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika kufanya kambi za mara kwa mara za upasuaji ili kuhudumia watoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news