Yanga SC yashusha kifaa kutoka Ghana

DAR ES SALAAM-Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Kimataifa wa Ghana, Hafiz Konkoni (23) kutokea Club ya Bechem United ya Ghana.
Hafiz katika msimu uliopita wa Ligi Kuu nchini Ghana alibuka nafasi ya pili kwa wanaowania Tuzo ya Mfungaji bora kwa kufunga magoli 15 na assist tatu katika michezo 26 aliyocheza.

Mshambuliaji huyo anakuwa mchezaji mpya wa nane baada ya mabeki Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate, Gift Freddy kutoka SC Villa ya Uganda, Kouassi Attohoula Yao,Peodoh Pacôme Zouzoua wote kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Wengine ni viungo Jonás Mkude kutoka Simba SC, Mahlatse Skudu Makudubela kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini na Maxi Mpia Nzengeli kutoka AS Maniema Union ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Aidha,inadaiwa Yanga SC wamempa mkataba wa muda wa miaka miwili hadi 2025 mshambuliaji huyo ambaye inatajwa kuwa ndio mbadala wa Fiston Kalala Mayele aliyeondoka katika timu hiyo na kuhusishwa kwenda Pyramid FC ya Misri.

Wakati huo huo, Kiungo wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Yanick Litombo Bangala amejiunga na klabu ya Azam FC kutoka Yanga.

“Tumefikia makubaliano na klabu ya Yanga ya kumnunua, mchezaji kiraka, Bangala na amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufuzu vipimo vya afya."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news