Daktari FEKI akamatwa Muhimbili

DAR ES SALAAM-Mkazi wa Dar es Salaam aliyejitambulisha jina la Mussa Mawa amekamatwa katika maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili akijihusisha kutapeli wananchi wanaopata huduma kwa kujifanya daktari.
Mkuu wa Idara ya Ulinzi,Bw. Alfred Mwaluko amesema kuwa wana usalama walimbaini daktari huyo feki akiwa kwenye harakati za kuwatapeli wananchi wanaouguza ndugu yao aliyelazwa jengo la Mwaisela.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Bw. Aminiel Aligaesha ametoa rai kwa watu wote wanaojihusisha na kutapeli wananchi katika eneo la Hospitali kwamba kwa sasa ulinzi umeimarishwa na wakijaribu kufanya hivyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya usalama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news