Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/2024 kuanza Agosti 15

DAR ES SALAAM-Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imetangaza rasmi ratiba ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/2024 utakaoanza Agosti 15, na kutamatika Mei 29, 2024.

Michezo ya ufunguzi itaanza Agosti 15 ikiwakutanisha Ihefu na Geita Gold uwanja wa Highland Estate, Namungo na JKT Tanzania uwanja wa Majaliwa na Dodoma Jiji dhidi ya Coastal Union uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Ligi hiyo itaendelea Agosti 16 kwa michezo miwili ambapo Mashujaa dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa Lake Tanganyika na Azam FC dhidi ya Kitayosce uwanja wa Azam Complex huku Agosti 17 Mtibwa Sugar itawakaribisha Simba uwanja wa Manungu Complex wakati Agosti 22, Singida BS itacheza na Tanzania Prisons uwanja wa Liti na mchezo wa mwisho wa raundi hii utawakutanisha Yanga na KMC uwanja wa Azam Complex Agosti 31.
Mchezo wa watani wa jadi wa Kariakoo unaokutanisha Simba na Yanga utachezwa Novemba 5 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni.

Akizungumza na waandishi wa Habari Afisa Mtendaji mkuu wa Bodi hiyo Almasi Kasongo amesema ratiba imezingatia ushiriki wa timu za Yanga, Simba, Azam na Singida BS kwenye Michuano ya kimataifa.

“Ugumu wa upangaji wa ratiba msimu huu umetokana na uwepo wa michuano ya kimataifa kwa ngazi ya Klabu na timu za taifa hivyo kusababisha ratiba yetu kuchelewa” alisema Kasongo.

Aidha Kasongo amesisitiza juu ya ubora wa viwanja vitakavyotumika kwenye Ligi Kuu msimu huu akisema Bodi haitasita kufungia kiwanja chochote endapo kitashindwa kukidhi ubora unaohitajika kikanuni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news