Prof.Muhongo kukagua miradi, kusikiliza kero za wananchi jimboni


NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo, anatarajia kukagua utekelezaji wa miradi ya maji ya bomba na kupokea kero mbalimbali za wananchi jimboni humo. 
Hayo yamebainishwa leo Agosti 4, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini. 

Aidha,taarifa hiyo imebainisha kuwa kamati ya Siasa ya Wilaya itaandamana na Mbunge kwenye ziara hizo mbili.

"Siku ya Jumatatu tarehe 7 Agosti 2023 mahalini Kijiji cha Bwasi saa 4 asubuhi. Saa 8 mchana Kijijini Mabuimerafuru. 

"Kamati ya Siasa ya Wilaya itaandamana na Mbunge kwenye ziara hizo mbili. Wote Mkarabishwa,"imeeleza taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news