Dkt.Yonazi:Tuongeze ushirikiano katika utendaji kazi

ZANZIBAR-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi amesema, ushirikiano wa kisekta katika ufanyaji kazi ni jambo zuri ambalo linaloleta ufanisi na ubora katika kazi ambazo zitakuza uchumi katika nchi na Taifa kwa ujumla 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara ya kujifunza utendaji kazi wa Idara ya Ufutiliaji na Tathmini ya Tume ya Mipango Zanzibar.

Ameyasema hayo baada ya kutembelea na kukagua miradi ya kimkakati iliyoko visiwani Zanzibar ambapo ametembelea mradi wa Bandari Jumuishi ulioko Mangapwani, Mradi wa Nyumba za Makaazi na Biashara pamoja na mradi wa nyumba za gharama nafuu. 
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini ya utendaji wa Serikalini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bi. Sakina Mwinyimkuu akiuliza swali wakati wa Ziara ya Kukagua Miradi ya Kimkakati iliyoko Visiwani Zazibar.

“Mimi ninaamini kwamba Taasisi zetu zitaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kutengeneza Uchumi imara katika eneo letu la Afrika Mashariki na Kati,na tukitambua kwamba soko letu linazidi kukua lakini sisi kama Nchi pia tuna fursa katika soko la SADEC kwa hiyo tukizingatie tunapakana na nchi nyingi hivyo tukitumia vizuri tunayo nafasi ya kujenga uchumi,”amesema Dkt.Yonazi.

Aidha,Dkt.Yonazi ameongeza kuwa Serikali imefanya uamuzi kuanzisha kurugenzi za Ufuatiliaji na Tathmini katika kila Wizara ambapo itasaidia Serikali kufuatilia miradi yake,mipango yake na kufaya maamuzi ya kiutendaji kwa wakati.
Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Dkt. Rahma Salim Mahfoudh akieleza namna ya Tume hiyo inavyofanya kazi.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Dkt. Rahma Salim Mahfoudh amesema jukumu la msingi la Ufuatiliaji na Tathmini Zanzibar ni kupanga na kufuatilia miradi ambapo kwa sasa wanampango wa muda wa kati ambao ni wa mwaka 2021 na 2026.
“Tuna miradi ya Kimkakati ambayo tunapoifanya inaongeza ufanisi katika kazi yetu na katika Miradi mliyotembelea leo ni Miradi ya kimkakati ya Nchi ambayo tunawapa sapoti kwa asilimia mia moja hasa kwa mradi kama shirika la nyumba ni fedha za serikali ambazo zimeingizwa ili kuufanya mradi ule,”alisema Katibu Mtendaji.
Baadhi ya Viongozi na Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wakati wa ziara Kukagua Miradi ya Kimkakati iliyoko Visiani Zazibar.(Picha na OWM).

Viongozi na Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wako visiwani Zanzibar kwa ziara ya siku mbili ya kujifunza utendaji kazi wa Idara ya Ufutiliaji na Tathmini ya Tume ya Mipango Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news