Rais Dkt.Samia atengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Mhandisi Nadhifa Sadiki Kemikimba.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 19,2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.

Mhandisi Kemikimba aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu mwezi Februari 2023, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu. 

Aidha,ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ubora wa Maji ambapo pia aliwahi kuhudumu katika idara hiyo kuanzia ngazi za kiufundi mpaka uongozi wa idara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news