Simba SC yajaza uwanja kabla

DAR ES SALAAM-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imeandika historia ya kuuza tiketi zote ndani ya siku tatu kabla ya mchezo.

Kwa mujibu wa uongozi wa Simba, maandalizi ya Simba Day yamekamilika ambapo tiketi zote 60,000 zinazojaza Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam zimeuzwa.

Aidha, hii inatajwa kuwa ni mara ya kwanza kwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kujaa siku tatu kabla ya tukio na Simba SC ndio wameweka historia.

Kwa mujibu wa Simba SC, Tiketi za Platnum ziliisha siku moja baada ya kutangazwa kuuzwa zikifuatiwa na VIP A siku mbili baadae.

Wakati huo huo, mageti ya uwanja yatafunguliwa mapema saa 2 asubuhi siku ya Jumapili ili mashabiki walionunua tiketi waingie mapema na kuondoa usumbufu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news