Watumishi walioghushi vyeti waitwa kulipwa malipo yao

MANYONI-"Kulikuwa na maagizo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan) ya kufanya malipo ya michango ya asilimia tano katika mifuko ya hifadhi ya jamii, kwa watumishi walioachishwa kazi kwa kosa la kughushi vyeti.

Hayo yamebainishwa na
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

"Naomba kutumia nafasi hii, kuwaomba sana na hasa watusaidie maafisa rasilimali watu, unajua wakati mwingine mtu aliyeghushi cheti ukimwambia njoo unipe taarifa zako, kwamba unatakiwa ulipwe kwa sababu kumbukeni kwamba kulipwa ni haki yao.

"Pamoja na kwamba hawa watu walikuwa na vile vyeti vya kughushi, lakini kwa namna moja au nyingine Manyoni hii ilipofika leo, wana mchango wao, wana jasho lao, kwa hiyo Mheshimiwa Rais kwa huruma yake, yeye kama mzazi alielekeza kwamba tutenge fedha kwa ajili ya kuwarudishia asilimia tano, ya michango yao ili nao wakienda huko katika maisha yao wawe na jambo la kufanya;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news