Wizara ya Afya yasisitiza jambo kwa TAHIA

DAR ES SALAAM-Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa Asasi ya TAHIA kutafakari juu ya kuwa na mfumo mmoja wa taarifa katika vituo vyote kuanzia ngazi ya Hospitali ya Taifa mpaka kwenye zahanati.

Lengo likiwa ni kusaidia kuokoa gharama za matibabu kwa mwananchi anayehitaji huduma hasa katika kipindi cha rufaa.

Dkt.Mollel amesema hayo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Asasi ya Tanzania Health Information Agency (TAHIA) inayoundwa na wataalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano yenye lengo la kuweka rasilimali watu pamoja, rasilimali fedha na teknolojia.

Ni ili kwa pamoja kuondoa changamoto iliyopo ya mifumo mingi inayoshindwa kubadilishana taarifa kutoka kituo kimoja kwenda kingine.

Amesema,mfumo huo wa taarifa za mgonjwa utaokuwa unasomana, utahusisha mpaka taarifa za fedha katika vituo, lakini pia huduma zinazotolewa kwa wagonjwa wanaotumia bima ya afya jambo litalosaidia kuboresha huduma kwa wananchi na kupunguza upotevu wa mapato katika vituo yanayofanywa na watumishi wasio waadilifu.

Aidha, Dkt. Mollel amesema, kuwepo kwa mfumo mmoja unaosomana katika Sekta ya Afya kutasaidia kuboresha matumizi ya taarifa (data) katika ngazi ya vituo na katika ngazi ya Viongozi wa juu wa Sera ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi ikiwemo kwenye eneo la kutenga fedha.

Sambamba na hilo, Dkt. Mollel ametoa onyo kwa wataalamu wanaolenga kutofautisha Sekta ya Afya katika utendaji na kusisitiza kufanya kazi kwa pamoja kwa kushirikiana ili kumhudumia mwananchi aliyechini bila changamoto yoyote.

Kwa upande mwingine, Dkt. Mollel amewataka Wadau katika Sekta ya Afya kupunguza fedha zinazotumika kwenye mafunzo, semina na warsha na kuelekeza bajeti kubwa zaidi kwenye maeneo yanayoonekana na kugusa zaidi changamoto za mwananchi wa chini mwenye uhitaji wa huduma.

Rais wa TAHIA, Bw. Sosthenes Bagumhe amemshukuru Mhe.Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel kwa ushauri alioutoa na kusisitiza tayari TAHIA imeanza kulifanyia kazi suala la kuunganisha mifumo na kuifanya iweze kubadilishana taarifa kwenye vituo kuanzia taifa mpaka zahanati ili kuondoa hadha kwa wananchi

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news