Adhabu yake ni kufukuzwa kazi-Waziri Simbachawene

NA RAINER BUDODI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, amewataka watumishi wa umma nchini kujiepusha na uhamisho usiozingatia taratibu za kiutumishi kwa kuwa ni kinyume cha maadili na adhabu yake ni kufukuzwa kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisikiliza hoja za watumishi wa umma wa Mkoa wa Geita katika kikao kazi chake na watumishi hao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo.

Mhe. Simbachawene ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa umma wa Mkoa wa Geita wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinawazokabili watumishi hao katika utekelezaji wa majukumu yao.
Sehemu ya watumishi wa umma wa Mkoa wa Geita wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo.

“Tumegundua kwamba kuna baadhi ya watumishi wanafanya uhamisho feki, wala sio wa Katibu Mkuu-UTUMISHI wala TAMISEMI, tumeanza kuwafuatilia na kuwakamata na tutaendelea kuwakamata kwa sababu ni watumishi wa umma na hawana pakukimbilia,” amesema Mhe. Simbachawene.

Waziri Simbachawene ameongeza kuwa, watumishi hao waliokiuka taratibu za uhamisho wanaweza kufanikiwa kudanganya mambo mengine yote na kwenda kwenye vituo hivyo vya kazi wanavyovitaka lakini hawatofanikiwa kuhamisha mshahara kutokana na udhibiti wa mifumo iliyopo.
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mji Geita, Bi. Pendo Daniel akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi wa umma wa Mkoa wa Geita kilicholenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo.

“Utahamisha kila kitu, lakini kinachokuja kusumbua ni kuhamisha mshahara kwa kuwa huwezi kuuona, kwani Mhe. Rais ameuficha, hakuna udanganyifu kwenye eneo hilo,” amesisitiza Mhe. Simbachawene.

Amewataka watumishi wote walioghushi uhamisho kurejea katika vituo vyao vya kazi vya awali vinginevyo hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa ikiwemo kufukuzwa kazi.
Afisa Mtendaji Kata ya Bombambili Halmashauri ya Mji Geita, Bw. Cosmas Bayaga akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi wa umma wa Mkoa wa Geita kilicholenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa mkoa huo.

Mhe. Simbachawene ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Geita yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma mkoani humo na kusikiliza changamoto za kiutumishi zinazowakabili ili kuzitatua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news