Afya Zanzibar, MSD wasaini mkataba kuimarisha upatikanaji bidhaa za afya

ZANZIBAR-Wizara ya Afya ya Zanzibar imetiliana saini mkataba wa makubaliano na Bohari ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya, hasa dawa visiwani humo.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Amour Suleiman Mohamed, amesema, mkataba huo ni muendelezo wa makubaliano ya muda mrefu kati ya Bohari ya Dawa Zanzibar (CMS) na Bohari ya Dawa nchini (MSD) ya kuimarisha upatikanaji wa huduma za dawa zenye ubora zaidi Tanzania.

Amesema, makubaliano hayo yamehusisha masuala mazima ya utaalamu wa kuwajengea uwezo watumishi, kuimarisha miundombinu ya Bohari ya Dawa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara, uhifadhi wa dawa na vifaa tiba pamoja na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Pia,ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imeweka vipaumbele vya kuimarisha huduma za afya ikiwemo masula ya dawa kama ilivyoanishwa katika mkataba huo.

Amesema, Wizara ya Afya kupitia Bohari ya Dawa itaendelea kushirikiana na MSD katika kutoa huduma bora za dawa hasa katika maeneo ya mifumo kwenye uagizajia dawa,vifaa tiba, uhifadhi na ununuzi wa dawa pamoja na kutafuta fedha kwa ajili ya kuwa na dawa za kutosha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavare Tukai amesema, MSD na Wizara ya Afya wana uhusiano wa kihistoria ambao umewezesha kuimarisha huduma za dawa kwa kubadilishana uzoefu, wataalamu pamoja na kusadiana kwa karibu pale inapotokea dharura.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news